Jumapili. 19 Mei. 2024

Mt. Fabiano, Papa na Mfiadini

Fabiano, Papa na Mfiadini

Mwaka 236 Mapadre na Wakristu wa Roma walikutana ili wamchague Papa. Njiwa alitoka Mbinguni akatua juu ya kichwa cha Fabiano. Watu wote waliokuwa hapo walistaajabu, lakini walitambua kwamba Fabiano ndiye aliyeteuliwa na Mungu kuwa Papa.

Alikufa kama Mfiadini wa Yesu Kristu baada ya miaka kumi na sita, wakati wa madhulumu ya Kaisari Desio, mwaka 250. Alizikwa karibu na Kaburi la Mt. Kaliisti.

Maoni


Ingia utoe maoni