Jumamosi. 18 Mei. 2024

Mt. ida, Bikira

ida, Bikira

Mt. Ida alizaliwa Ireland. Kijana mmoja wa familia maarufu alimwomba baba wa Ida ili amwoe binti yake. Ida akafunga na kusali siku tatu, ndipo baba yake akampa ruhusa aishi maisha ya ubikira.

Alikusanya kikundi cha wasichana na kuendesha shule ya watoto wadogo. Mmoja wao alikuwa Mt. Brendan, ambaye alimfundisha muda wa miaka mitano, na baadaye akawa abati na mmisionari maarufu. Watoto walifundishwa hasa vitu vitatu:

Kwanza, Imani kwa Mungu, na kuwa na moyo safi.
Pili, maisha ya kawaida, na roho ya kumcha Mungu.
Tatu, ukarimu unaoletwa na upendo.

Baada ya miaka mingi ya kumtumikia Mungu na kuwahudumia jirani, Mt. Ida alikufa mnamo mwaka 570.

Maoni


Ingia utoe maoni