Jumamosi. 18 Mei. 2024

Mt. Sava wa Serbia, Askofu

Sava wa Serbia, Askofu

Sava alizaliwa 1175, akiwa mtoto wa kiume wa tatu wa Stefano wa kwanza, Mfalme wa Serbia (Yugoslavia). Alipokuwa na umri wa miaka kumi na saba alijiunga na wamonaki wa mlima Athos (Ugiriki). Baada ya miaka minne baba yake alijiunga naye kisha kujiuzulu ufalme. Yeye na baba yake walianzisha nyumba ya utawa kwa ajili ya wamonaki wa Kiserbia. Na nyumba hii ipo hadi ivi leo, na ni moja ya monasteri kumi na saba zilizo maarufu sana mjini Athos. Alianza kazi ya kutafsiri vitabu katika Lugha ya Kiserbia. Hata hivi leo vipo vitabu vya zaburi na Ibada alivyoandika mwenyewe, ambavyo vinalindwa kwa heshima katika monasteri ya Kilandari kule Athos ambavyo vimetiwa saini: "Mimi monaki Sava asiye na thamani na mvivu".

Mwaka 1208 padre Sava alirudi Serbia na ndiye aliyekuwa Askofu Mkuu wa kwanza wa nchi hiyo. Mara kwa mara aliondoka kwenda kukaa porini ili apate nguvu za kuendelea na kazi yake. Wakati alipokuwa akirudi safarini, alikufa Bulgaria tarehe 14 Januari, 1237, akiwa na uso wenye furaha. Askofu Sava ni msimamizi Mtakatifu wa watu wa Serbia. Yeye huheshimiwa na Wakristu wa Madhehebu ya Ortodoksi na kadhalika wa Kanisa Katoliki la Roma.

Maoni


Ingia utoe maoni