Abo, Mfiadini
Mt. Abo alizaliwa Bagdad (Iraki). Alikuwa kijana wa kiarabu na Mwislamu, ambaye wakati wa ujana wake aliingia kazi ya kumtengenezea marashi mtoto wa Mfalme wa Georgia katika nchi ya Urusi. Alipokuwa Tibilisi aliutambua wazi ukweli wa dini ya Kikristo, lakini aliogopa kujitangaza mwenyewe kwa sababu Georgia ilikuwa ikitawaliwa na Waislamu.
Wakati mwajiri wake alipoenda kuishi, kama mkimbizi, kwenye sehemu za kaskazini na Ziwa Kaspian, Abo alifuatana naye, na huko akabatizwa. Mwaka 782, walirudi Tibilisi, na baada ya miaka kadhaa Abo alifikishwa mbele ya hakimu wa Kiislamu. Naye akakubali kuwa ni kweli ameasi. Baada ya kukaa kifungoni muda mfupi, walimkata kichwa. Sikukuu ya Mt. Abo inatukuzwa na Wakristu katika nchi ya Urusi.
Maoni
Ingia utoe maoni