Rigoberti
Rigoberti aliishi karne ya sita katika nchi ya Ufaransa. Miaka kadhaa baada ya kuwa abati wa Wabenediktini, aliteuliwa kuwa askofu mkuu wa Remsi (Reims, Ufaransa). Mkuu wa Ikulu ya Mfalme wa Ufaransa, aitwaye Karoli Martel, alimsumbua na hata kumtesa Askofu Rigoberti. Huyo Karol Martel alikuwa mtu jahili. Kwa maoni yake, Askofu Rigoberti alikuwa amekosa msimamo wake, aka mpeleka mbali, na mamlaka yake ya kiaskofu alipewa Askofu Milo aliyekuwa anatawala jimbo la Tria (Trier, Ujerumani)
Baadaye Askofu Milo na Askofu Rigoberti walisikilizana vizuri, na hivyo, Askofu Rigoberti aliruhusiwa kurudi na kuishi kwenye kiwanja chake kidogo karibu na Remsi. Aliishi huko akifanya mafungo ya roho, na kusali, akivumilia kwa unyenyekevu aibu ya mabezo yake, bila kumchukia mtu yeyote. Mojawapo ya furaha zake ilikuwa kujitokeza mara moja katika kanisa lake kuu ambapo Askofu Milo alimruhusu kuendesha baadhi ya Ibada. Mtakatifu Rigoberti alifariki dunia mwaka 750.
Maoni
Ingia utoe maoni