Jumatano, Aprili 24, 2019
Jumatano, Aprili 24, 2019.
Oktava ya Pasaka
Mdo 3:1-10
Zab 105:1-4,6-9
Lk 24:13-35
UFUFUKO: YESU YUPO HAI KATIKA EKARISTI TAKATIFU.
Kutokea kwa Yesu kwa wafuasi wake wawili inaonekana kuleta hisia. Walikuwa wameshakuwa na matumaini kwamba yeye ni Masiha lakini aliuawa. Na tazama kuna wengine wanasema kaburi lake liko wazi. Kadiri ujumbe unapo endelea, Yesu “anawaelezea yote yaliosemwa kuhusu yeye katika maandiko”. Kwa njia hiyo wale wafuasi wakatambua huyu mtu wanaye ongea naye ana uelewa wa juu na hekima ya hali ya juu, hivyo wanamualika akae nao. Yesu alikaa na kuketi nyumbani kwao. Wakiwa pale, maandiko yanasema “alichukua mkate, akaubariki, akaumega na kuwapa. Kwa njia hiyo macho yao yalifumbuliwa, wakamtambua na ghafla akaondoka machoni mwao”. Kwanini Yesu, alificha wafuasi wake wasimtambue alikuwa nani, na kuwaruhusu wamtambue tu, na ghafla akaondoka machoni mwao?
Yesu alipenda wale wafuasi na sisi wote pia, kwamba huyu ambaye amefufuka kutoka wafu yupo hai kweli na kwamba tutamtambua katika kuumega mkate. Tutamtambua katika Ekaristi Takatifu. Kutokea kwa Yesu kwa wafuasi wake, ni wazi, kwamba Yesu anakuwa wazi katika Ekaristi Takatifu. Yesu yupo hai katika Ekaristi! Lakini inatuambia kuwa amejificha ndani ya Ekaristi Takatifu. Muunganiko huu wa kujificha na uwepo wake kweli unatupa muongozo mzuri wa Imani yetu.
Wafuasi walikuwa mbele ya Yesu lakini hawakuweza kumtambua. Pengine na sisi ni wazi pia. Hili ni kweli hasa wakati tukiwa kanisani wakati wa misa lakini pia kwa upande mwingine tunamtambua. Tunapaswa kujikita katika kumuona yeye, kumtumbua na kumwabudu. Tunapaswa kutambua uwepo wa Yesu mfufuka kati yetu. Yupo nasi sasa, anatupenda sisi, anaongea na sisi, na anatuita tumpende. Tumtafute na kusikiliza sauti yake. Unaweza kushangazwa ni kwa jinsi ghani anaweza kuwa.
Sala:
Bwana, ninakushukuru kwa kunipenda mimi kila wakati. Ninaomba unipe macho ya Imani niweze kukuona daima katika Ekaristi Takatifu, na naomba unisaidie niweze kutambua uwepo wako katika kila tukio la maisha yangu. Ninakupenda, Bwana mpendwa. Yesu, nakuamini wewe.
Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni