Jumanne. 26 Novemba. 2024

Tafakari

Jumamosi, Aprili 13, 2019

Jumamosi, Aprili 13, 2019,
Juma la 5 la Kwaresima

Ez 37: 21-28;
Yer 31: 10-13;
Yn 11: 45-56


KUJITAZAMA KIDOGO NA KUMTAZAMA YESU ZAIDI!
Katika Injili ya leo tunaona jinsi Kayafa kuhani mkuu anavyo fikiri. Maneno yake yanavutia katika hali kwamba ni ya huzuni lakini yanatoa unabii kwa wakati mmoja. Walitamani na wanaanza kupanga yeye na makuhani wengine pamoja na Mafarisayo jinsi ya kumkamata Yesu na kumuua. Lakini kinachotupa kitu ni jinsi ya msukumo wa Kayafa na wengine.

Yesu alikuwa akipata umaarufu na walikuwa wakiogopa umaarufu wake utachochoea vitu kati ya Warumi. Na walikuwa na wivu kwamba Yesu amewavutia watu wengi sana. Na Kayafa anatoa mantiki iliojificha kwamba inapaswa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu kuliko taifa zima liangamie. Kwa maneno mengine alifikiri kwamba kwasababu Yesu anapata umaarufu sana na kwasababu watu wengine walikuwa wakimsikiliza Yesu zaidi kuliko wao makuhani na mafariyo, ni kwamba “ni vizuri kuliondoa tatizo” ili mambo yaweze kuendelea kama yalivyo zoea.

Hili linafunua ukweli kwamba Mafariyo walikuwa wakijali zaidi nafsi zao na umaarufu wao kuliko ukweli. Kama Mafarisayo na Makuhani walikuwa wanapenda ukweli, wangeona pia utukufu na mamlaka aliokuwa nayo na kumwamini yeye na kumfuata. Lakini hawakuweza kuacha majivuno yao na kukubali ukweli na kumfuata mtu mwingine badala ya nafsi zao. Hawakuweza kuachia mamlaka yao.

Hali hii pia tunaiona katika maisha yetu ya kila siku. Mara nyingi tunataka sisi tuwe kitovu cha kuangaliwa. Na mara nyingi tunavyo muona mtu mwingine akifanya vizuri au akipokea sifa tunapatwa na wivu mbaya. Na wivu wetu unageuka na kuwa chuki. Tuna enda mbali na Yesu pia. Tujaribu kufikiria muda tuliokuwa tukifanya kama Kayafa. Na tunapo ingia katika wiki kuu, tuelekeze macho yetu kwa Yesu kuliko kwa nafsi zetu. Tujikute sisi wenyewe chini ya mslaba wake siku ya Ijumaa kuu kwa mapendo na ujasiri, tukisimama karibu na tukimpenda katika njia zetu zote za maisha.

Sala:
Bwana, ninaomba nikufuata wewe katika wiki kuu inayokuja. Ninakuomba niwe na upendo wa kukupenda wewe hata katika kukataliwa kwako na uchungu. Ninaomba unisaidie nitupilie mbali wivu na chuki na kukuona wewe katika mateso ya wengine na katika furaha yao. Yesu, nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni