Jumatano, Aprili 03, 2019
Jumatano, April 03, 2019.
Juma la 4 la Kwaresima
Isa 49: 8-15;
Zab 145: 8-9, 13-14, 17-18;
Yn 5:17-30
FURAHI KATIKA MAPENZI YA MUNGU!
Kama mtoto wa Yosefu mseremala, alijifunza ni nini baba yake alipenda. Muda baada ya muda alikuja kuelewa zaidi, jinsi ya kunyoosha au kukata vipande viwili na kuviunganisha. Alianza kuona kazi iliomalizika ya baba yake, kuona meza au kiti alicho tengeneza baba yake. Na mwisho pengine aliweza kutengeneza kama baba yake na kumfanya baba yake afurahi. Leo katika Injili Yesu anaongea na Baba yake wa Mbinguni katika hali ya mfanano kama hiyo. Anasema na kufanya yale malengo ya Baba yake. Kwasababu ameyaweka malengo yote moyoni mwake. Anatambua kabisa katika hali zote ni kwa ajili ya ukombozi.
Kwa upande wetu, tunaweza kuchukua uelewa wa umoja huu wa Baba na Mwana, somo la utukufu jinsi ya kuingia katika umoja huu na Mungu. Pili, tunapaswa kuamini tunacho elewa, na tukichague kwa ajili ya maisha yetu. Changamoto ni kwamba kuna sauti nyingi zinazo tuita na kushindana na maamuzi yetu. Tukiwa tunachagua kati ya hizo, kuchagua tu ile ambayo Mungu anatufunulia, tunakuwa tunavutwa moja kwa moja kwa mapenzi ya Mungu na kuyafanya. Kwa njia hii sisi nasi tunakuwa wamoja na Mungu.
Kama Yesu, sisi wote tunataka kufanya mapenzi ya Mungu. Lakini ili kuwa wenye mafanikio katika kazi zetu tunapaswa kutambua picha yote. Mara nyingi tunachoka tukijaribu kuchagua vitu vidogo, kwamba sijui Mungu atapenda nibaki katika familia yangu jioni hii au niende kwenye mkutano parokiani. Ni wazi Yesu anajali kila kitu katika maisha yetu, lakini tutajikuta ni rahisi kufanya uchaguzi sahihi wakati tukiwa na uelewa mkubwa juu ya nini Baba anatengeneza na ni kwa jinsi ghani anatualika kila mmoja wetu kuingia katika malengo yake makubwa.
Sala:
Baba wa Mbinguni, ninakushukuru kwa zawadi ya Yesu Mwanao na ninakushukuru kwa umoja mlionao. Nivute katika utukufu uliopo katika kuyafanya mapenzi yako. Nifanye mmoja wako, uendelee kuwa Baba yangu daima. Baba wa Mbinguni, Yesu Mwana wa Mungu, nakuamini wewe.
Amina .
Maoni
Ingia utoe maoni