Jumapili. 24 Novemba. 2024

Tafakari

Jumatano, Oktoba 12, 2016

Jumatano, Oktoba 12, 2016,
Juma la 28 la Mwaka wa Kanisa

Gal 5:18-25;
Zab 1:1-4, 6;
Lk 11:42-46


KUJIZOESHA KUTENDA FADHILA!

Katika somo la kwanza leo Mt. Paulo leo anaorodhesha baadhi ya vitu ambavyo Wagalatia wanapaswa kuepuka. Anasema kuna baadhi ya matendo ya mwili. Pengine ni kama tunavyosikia baadhi yake ni, mumonyoko wa maadili, uasherati, kuabudu miungu mingine, ushirikina, ulevi na anasa, tunaweza kujisifia na kusema, Oh! Mimi sitendi kati ya hayo. Hii inaweza kutufanya turidhike na kujiona bora kuliko wengine. Lakini hata hivyo, tukipitia hiyo orodha kwa makini na kwa ndani kabisa, tunaweza kutambua kwa namna moja au nyingine tunahitaji Roho wa Mungu zaidi ili tuweze kuwa wema na kuepuka hayo.

Yesu anawataja walimu washeria na Mafarisayo kwa maneno makali kabisa. Yesu anatumia mfano wa zaka kuonesha ni kwa jinsi ghani walivyotoka njee ya mstari. Mungu alitaka sadaka ya mazao ya kwanza kama shukrani na heshima ya nguvu zake kwa kujali watu wake (Kumb. 14: 22; Lev. 27: 30).

Waandishi walienda mbali zaidi na kuwatoza watu zaidi tena kwa kutumia mahesabu na ujazo usio wa muhimu, na kushindwa kuwajali maskini na wahitaji. Walishikwa na wivu na kushindwa kuwapenda wengine. Yesu pia anawalinganisha pia na “makaburi yasio na mipaka” ilikuwa mtu akijigusa na kaburi alikuwa anatiwa najisi kwa muda wa siku saba (Hes 19:16). Wale wote waliokuja kuwasikiliza Mafarisayo na waandishi kadhalika walitiwa unajisi kwa mafundisho yao ya uongo.

Kiini cha amri za Mungu ni upendo. Mungu ni Upendo na kila kitu anchotenda kinatoka katika upendo wake kwetu sisi. Je, una ruhusu Upendo wa Mungu ubadili akili yako na moyo wako? Je, upo tayari kukuwa katika fadhila katika upendo kwa Mungu na jirani? Fadhila inapaswa kupaliliwa kwa sala na matendo mema ili zikuwe na zimee ndani kabisa mwa mioyo yetu, ili ziweze kukomaa na kuchanua. Kama vile mimea inavyo hitaji maji na mbolea ili imee vizuri, ndivyo na fadhila za Kimungu zinapaswa kumwagiliwa kwa kuzitenda kila wakati na kuwa karibu zaidi na Mungu. Tumuombe Mungu atusaidie kusogea karibu naye daima, kadiri unavyokuwa karibu na taa ndivyo uhakika wakuona unakuwepo. usaidie kusogea karibu naye daima, kadiri unavyokuwa karibu na taa ndivyo uhakika wakuona unakuwepo. Tuishi kama Mungu anavyopenda ili tutende kwa upendo kama Mungu anavyotutendea.

Sala: Bwana, washa ndani ya moyo wangu kwa upendo ili niweze kutenda yale yalio ya lazima kabisa-Upendo kwa Mungu na Upendo kwa Jirani. Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni