Jumanne, Machi 12, 2019
Jumanne, Machi 12, 2019,
Juma la 1 la Kwaresima
Isa 55:10-11;
Zab 34: 4-7, 16-19;
Mt 6: 7-15
KUJIFUNZA KUSAMEHE!
Mara nyingi, kipindi cha kwaresima ni kipindi ambacho katika mwaka tunapima afya zetu za Kiroho, lakini pia ni wakati ambapo tunapaswa kuangalia, kama tunajiangalia zaidi nafsi zetu kuliko kumwangalia Mungu wetu anayetupenda. Kwaresima ni kipindi cha kuangalia kama Mungu anachukua nafasi ya Kwanza.
Mt. Augustino alisema: Sala ya Baba yetu, ni kamilifu kabisa kiasi kwamba inafupisha kwa maneno machache yote ambayo mwanadamu anataka kumwomba Mungu. Mzizi wa sala hii ni MSAMAHA. Kusamehe na kusamehewa. Yote yanapaswa kutamaniwa na kutafutwa. Pengine changamoto iliopo katika kusamehe wengine ni hali ya “haki” ambayo inaonekana kupotea baada ya msamaha kutolewa. Hili ni kweli hasa kwa mtu ambaye anasamehewa ambaye ameshindwa kuomba msamaha. Katika hali nyingine wakati mmoja ameomba msamaha, na kuonesha kutubu, ni rahisi kusamehe. Lakini wakati aliyekosea haoneshi hali ya kutubu wala kujuta, hili linaacha hali ya kuoneakana kama kuna ukosefu wa haki wakati msamaha unapotolewa. Na hili linaweza kuwa ngumu sana kwetu kulishinda.
Kuwasamehe watu hakumanishi unaifuta dhambi. Msamaha haina maana kwamba dhambi haikutendwa au kwamba ni sawa tu imetokea. Bali, kumsamehe kunatenda tofauti. Kusamehe ni wazi kwamba kunaionesha dhambi yenyewe, kuikubali na kuona jinsi ya kuachana nayo. Hili ni muhimu kulielewa. Kwa kuitambua dhambi ambayo inapaswa kusamehewa, alafu na kuisamehe, haki inatendeka katika hali ya Kimungu. Haki inatendeka kwa njia ya huruma. Na huruma ina msaidia anayetoa msamaha zaidi kuliko yule anayepokea. Kwa kuona huruma kwa dhambi ya mwingine, tunakuwa huru kwa madhara ya dhambi ya mwingine. Huruma ni njia ya Mungu ya kuondoa maumivu haya katika maisha yetu na kutuweka huru tuweze kutambua huruma yake zaidi kwa msamaha wa dhambi zetu wenyewe, huruma ambayo hatuwezi kusema tunaipata kwa jitihada zetu wenyewe tu.
Tutafakari leo, kuhusu mtu ambaye kweli unataka kumsamehe. Ni nani na alifanya nini kukuumiza? Usiogope kuwa na huruma na kumsamehe wala usisite kufanya hivyo. Na kwa huruma utakayotoa italeta haki ya Mungu katika hali ambayo kwa nguvu zako mwenyewe huwezi kuitimiza. Kwa kitendo cha kusamehe kinakufanya kikuweke huru kwa mzigo wa dhambi, na kumfanya Mungu akusamehe wewe makosa yako.
Sala:
Bwana, mimi ni mdhambi ninaye hitaji huruma yako. Ninapo tafuta huruma yako, nisaidie pia niwasamehe wengine kwa madhara walio nitendea. Yesu nakuamini wewe.
Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni