Jumanne. 26 Novemba. 2024

Tafakari

Jumapili, Machi 10, 2019

Jumapili, Machi 10, 2019.
Jumapili ya 1 ya Kwaresima

Kumb. 26:4-10
Zab. 91:12, 10-15 (K) 15
Rum. 10:10-13
Lk. 4:1-13

VISHAWISHI-NAFASI YA KUKUWA!
Kushawishiwa , maana yake ni kuvutwa kwenye kitu kisichoruhusiwa. Injili ya Leo inatuambia Yesu alijaribiwa “Kristo kuhani Mkuu, alijaribiwa kwa kila namna kama tulivyo lakini hakutenda dhambi” (Ebr 4:15). Biblia inatualika tutazame vishawishi kama nafasi ya kujipima uchaguzi wetu, nafasi ya kukuwa. Uchaguzi upo kati ya kukubali mpango wa Mungu au kuukataa. Adamu aliamua kuchagua njia isiofaa/hukumu yake mwenyewe; Kristo daima alirejea neno la Mungu daima. Adamu alinyoosha mkono wake juu ya tunda la kifo; Yesu amekuwa chanzo cha uhai.

Katika somo la Injili, “Yesu alikaa jangwani kwa siku arobaini na alijaribiwa na shetani” (Mk 1:12-13). Kwa kutumia lugha ya Biblia na lugha ya picha, alimaanisha maisha yote ya Yesu yalikuwa kati yake na huku shetani akimjaribu. Majibu ya Yesu kwa shetani yanawakilisha matukio matatu ya wana Waisraeli katika kitabu cha kutoka: manunguniko ya chakula na zawadi ya manna (Kut 16), kugoma kwasababu ya maji (Kut 17), kuabudu ndama wa shaba (kut 32) hivyo Yesu anayaishi tena maisha ya watu wake. Yeye anapatwa na majaribu yale yale, lakini anayashinda. Ni wale tu, wanaothamini maisha yao katika mwanga wa neno la Mungu wanaoweza kutoa ushuhuda wa kweli Ulimwenguni.

Vishawishi vipo. Ni matokeo ya maanguko ya wanadamu wa kwanza. Yanatoka katika udhaifu wetu lakini pia kutoka katika yule muovu. Yesu hakukubali kuanguka katika vishawishi alivyokuwa jangwani na wala hakuanguka katika kishawishi katika maisha yake yote. Aliyashinda na kuteseka kwa ajili ya hayo. Hili linatuambia kwamba anaweza kuwa kiongozi wetu na mfano wetu wa kuiga wakati tukiwa katikati ya vishawishi kila mara na kila siku. Wakati mwingine tunaweza kujisikia wa pweke tuliotengwa katika jangwa la dhambi zetu. Tunaweza kujisikia kama vile mnyama mkali wa tamaa zetu unatushinda. Tunaweza kujisikia yule muovu anatunyemelea. Sawa, Yesu alipatwa na haya pia. Aliruhusu kupitia haya kwa kushiriki ubinadamu wetu. Kwa njia hii ni Yesu anayeweza kukutana nasi katika jangwa letu. Yupo tayari anatusubiri, akitutafuta, akituita sisi. Ni huyu alieyeshinda vishawishi vya muovu jangwani, ndiye atakaye tuongoza kuepuka. Kwahiyo, kama jangwa lako ni mahangaiko ya maisha sasa, au ni majaribu mbali mbali, Yesu anataka kukutana nawe akuongoze katika njia iliyo njema. Alimshinda yule wa jangwani na jinsi alivyokuwa, hivyo anauwezo wakushinda jangwa lolote lile katika maisha yako.

Sala:
Bwana, ninakubali upendo wako mkamilifu kwangu. Nina amini kwamba unanipenda mimi kiasi kwamba nitaweza kuvumilia mateso, kuelewa mateso yote. Ninakuomba nikutane nawe katika jangwa la maisha yangu. Ninakuomba nikuruhusu wewe uniongoza katika sehemu tulivu na yenye maji. Yesu nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni