Jumamosi, Machi 02, 2019
Jumamosi, Marchi 2, 2019,
Juma la 7 la Mwaka wa Kanisa
Kumbukumbu ya Bikira Maria
YbS 17: 1-15;
Zab 103: 13-18;
Mk 10: 13-16.
KAMA WATOTO WADOGO!
Yesu anatumia mfano wa watoto kuelezea jinsi ya kupokea ufalme wa Mungu. Tunapaswa kuupokea kama mtoto. Sio kwa wasi wasi na mashaka, bali kwa uwazi, furaha na unyenyekevu.
Ulimwengu tunaoishi unaelekeza sana kwenye dhambi na kuelekeza vibaya tamaa za mwanadamu. Uovu unatawala katika familia zetu kiasi kwamba karibia tutanawaona wenzetu kuwa kama kifaa fulani cha kutamani tu. Hili linaoneakana zaidi katika matangazo yetu ya Tv na hata katika filamu mbali mbali. Tamaa ya kupata vitu na watu ni kubwa sana na inawakumba watu wengi kiasi kwamba watu wanaishia kutafuta mali kwa nguvu hata katika hali ya uhalifu. Moja ya matokeo ya hili nikwamba tunapoteza upendo wa kibinadamu. Na matokeo yake, uelewa wa upendo wa kweli ya kibinadamu unapotea.
Katika injili ya leo Yesu anasema “Waacheni watoto waje kwangu. Anawakumbatia watoto na kuwabariki kwa kuwawekea mikono”. Mstari huu unafunua kwetu Utakatifu, uhalisia na upendo aliokuwa nao Yesu kwa hawa watoto na sisi. Ingawaje, sio watoto tu waliokuja kwake. Hata wanawake wadhambi waliibusu miguu yake na pia hata Yohane mtume, alilaza kichwa kifuani kwake wakati wa chakula cha mwisho cha jioni.
Upendo wa kibinadamu unapaswa kutakaswa na kuwekwa katika hali ya kwamba tunautoa kwa wanadamu wenzetu bila kuwa na mtazamo mmbaya. Wakati linaweza kufanyika, kama Yesu alivyofanya, kama vile mzazi aweza kuwakumbatia watoto wake, rafiki kwa rafiki, mwana ndoa kwa mwana ndoa n.k. inakuwa ni hali ya utakatifu na uhalisia wa kueleza upendo katika moyo wa Kristo.
Tutafakari juu ya uzuri wa upendo wa kibinadamu. Tutafakari juu ya tamaduni zetu zinazo jaza mtafaruku na hali ya kuchanganyikiwa katika hali ya kawaida ya kuoneshana upendo wa kibinadamu. Tumuombe Mungu atuondolee ile hali ya kudhaniana vibaya, inayozuia pia wakati mwingine tushindwe kusalimiana kindugu na kwa upendo wa kibinadamu. Tuombe pia kwa zawaidi ya usafi wa moyo ili Bwana wetu aweze kuwakaribisha wengi kwakwe kwa kupitia mioyo yetu kwa upendo.
Sala.
Bwana, nisaidie niweze kuwa msafi rohoni. Nisaidie mimi niweze kukuruhusu wewe kutakasa mapendo yangu ili uweze kungaa ndani yake. Nikinge mimi na mtazamo mmbaya wa vishawishi vya tamaduni tunazoishi na unisaidie niweze kuonesha mapendo yako. Yesu, nakuamini wewe.
Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni