Jumanne. 26 Novemba. 2024

Tafakari

Alhamisi, Februari 14, 2019

Alhamisi, Februari 14, 2019,
Juma la 5 la Mwaka wa Kanisa

Mwa 2: 18-25;
Zab 128: 1-5;
Mk 7: 24-30.


KUDHIHIRISHA IMANI!
Kwanini Yesu anaongea na Mwanamke yule kwa jinsi ile? Mwanamke anakuja kwake, pengine katika hali ya hofu, na kuanguka katika miguu yake, nakuomba amponye mtoto wake. Anamwambia “si haki kuchukua chakula cha watoto na kutupia Mbwa?” Kwanini alisema hivi?

Kwanza kabisa, tunapaswa kufahamu kila anachosema Yesu ni kitendo cha upendo. Ni kitendo cha huruma kuu na ukarimu. Tunafahamu hivi kwasababu ndivyo Yesu alivyo. Yeye ni upendo wenyewe. Sasa twawezaje kupatanisha mchanganyo huu? Ufunguo wa kufahamu mchanganyo huu ni kutazama matokeo yake. Tunapaswa kuangalia jinsi huyu Mwanamke alivyo mjibu Yesu na jinsi mazungumzo yalivyo isha. Tukifanya haya, tunaona kwamba mwanamke huyu amejibu kwa imani na unyenyekevu mkubwa. Anachosema Yesu ni ukweli, tunaweza kusema kwamba alichosema ni kwamba hakuna mwenye haki ya huruma yake na neema. Hakuna, kwa mama yule pamoja na mtoto wake, ya kwamba “wanastahili” Mungu kufanya kazi katika maisha yao. Yesu anatambua hili, na kwa kusema alichosema, alimpa mama huyu nafasi ya kuonyesha imani yake kubwa ili wote waweze kuona. Kwa maneno yake yalimfanya angae kwa imani yake, matumaini na kuamini. Hili ndilo lilokuwa lengo la Yesu na kweli lilifanikiwa. Lilifanikiwa kwasababu alivyokuja kwa Yesu, Yesu alitambua kwa hakika alikuwa na imani kubwa. Alifahamu atajibu kwa unyenyekevu na kwa imani. Mwanamke huyu alifanikiwa na sisi pia tunaweza kushuhudia juu ya imani yake kubwa na unyenyekevu.

Tujitahidi kujiweka kwa viatu vya mwanamke huyu na tumsikie Yesu akiongea maneno haya haya kwetu. Je, utajibu nini? Tutajibu kwa hasira na chuki? Je, majivuno yetu yataumizwa? Au tutajibu kwa unyenyekevu wa ndani, na kutambua kuwa kila tunachopokea kwa Mungu ni zawadi na kwamba sio haki yetu? Kujibu namna hii ni kitendo cha imani ambayo Mungu anaisubiri kutoka kwa kila mmoja wetu na ni ufunguo wa kupokea huruma yake tunayo hitaji.

Sala:
Bwana, naomba uninyenyekeshe. Tupa mbali majivuno yangu. Nisaidie niweze kuanguka miguuni mwako. Nisaidie niweze kukusadiki kwamba umependezwa na mapendo yangu kwako, ufungue wingi wa neema zako na kumimina juu yangu. Yesu, nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni