Jumapili, Februari 03, 2019
Jumapili, Februari 03, 2019
Dominika ya 4 ya Mwaka
Yer 1: 4-5,17-19;
Zab 71: 1-4;
1 Kor 12:31, 13:1-13;
Lk 4:21-30.
------------------------------------------------
NABII:MWANGA KWA ULIMWENGU
Hakuna hata mmoja wetu anayependa kusikia ukweli hasa pale yanapoeleza kitu ambacho sio kizuri katika maisha yetu. Leo katika somo la Injili tunashangaa tukio la Yesu kufukuzwa katika hekalu la nyumbani kwake kabisa kuzaliwa, Nazareth.
Katika somo la kwanza tunasikia kuhusu Yeremia ambaye ni nabii mkubwa ambye Mungu alimtuma kati ya watu wake. Tunasikia wito wake alioitiwa na Mungu na anayopaswa kufanya kama nabii. Katika somo la pili tunasikia Paulo akiwa katika wimbo mkuu wa upendo. Anatuambia kwamba kuwa mfuasi wa Kristo Upendo ni fadhili kuu kabisa kuliko yote. Katika Injili tunamsikia Yesu akishirikisha kuhusu nabii wa kweli kukataliwa na watu wa nyumbani kwake mwenyewe.
Tunaposikia kuhusu nabii mara moja kitu kinachokuja kichwani ni mtu ambaye anaweza kututabiria kuhusu mambo yajayo mbele. Lakini hili sio maana halisi ya Kibiblia, nabii maana yake ni mtu ambaye anaongea kwa niaba ya Mungu. Huyu ni mtu ambaye katika hali ya Kimungu anaweza kuyaona mambo kama yalivyo na bila kujaribu kuyapindisha. Kuwa tayari kuyaeleza kama yalivyo.
Mara nyingi nabii hawi maarufu kwa watu wake mwenyewe. Sio kwamba haoni mambo kama yalivyo bali nikwasababu anaona mambo jinsi yalivyo na anawaambia ukweli. Kwa njia nyingine , ana ujasiri wa kuwambia ukweli. Anathubutu kusema ukweli wa mambo yale ambayo watu wengine wanaona kama ni kweli ndani kabisa ya mioyo yao lakini hawasemi. Hawataki kukumbana na ukweli kwasababu wanaona yanatisha na yana gharimu. Nabii yeye huyasisitiza na kuyasema kama yalivyo. Yeye huzima majifanyo yetu na kuanika ukweli. Tunaposhindwa kupokea ujumbe, tunamfukuza mjumbe. Kusikiliza ujumbe wa nabii ni dalili ya kukubali kwamba tunakosea na tupo tayari kubadilika.
Mfano mmoja, Siku moja kulikokuwa na kundi la watu ambao walitishiwa huku duniani wakaamua kukimbilia kwenye pango fulani na kuamua kujificha huko. Walikaa huko na kuzoea kiasi ambacho waliona lile giza la ndani ya pango kama ukuta kwao. Walikuwa na muda tuu wa usiku wakutoka na kwenda kujitafutia chakula. Walikaa ndani kiasi ambacho walijifunza kuona kwenye giza. Waliangalia watu wa njee na kuona mazingira yao kama yanatisha na hata wakaanza kuwaonea huruma. Walijidanganya kiasi ambacho wao wenyewe walijiona kama waliochaguliwa na Mungu kutoka katika ulimwengu huo. Kwamba Mungu amewachagua watoke katika ulimwengu huo mbaya. Walifunga macho juu ya ukweli wa maisha yao, wakawa vipofu kwa ulimwengu wao, na kuendelea kuishi katika hofu ya daima.
Haya yaliendelea hadi pale mmoja wao kijana mdogo alivyo amua kuondoka na kwenda kutafuta mwanga.
Walimuangalia kama msaliti wao na mbaya sana. Huyu kijana mdogo alitambua mara moja kwamba ulimwengu ulionjee ni tofauti kabaisa na ulimwengu aliofundishwa. Na wala sio sehemu ya kutisha kama alivyoambiwa. Ni kweli wakati mwingine kuna mambo machache ambayo sio mazuri yanatokea pale lakini ni ulimwengu ambao jua huangaza, na kupambwa na harufu nzuri ya maua. .Ulimwengu uliopambwa na sauti za ndege na vicheko vya watoto wadogo wakicheka. Kijana huyu akachukulia kama ndege mdogo anayeacha kiota na kupaa juu ya anga. Alifanya nini? . alitoka na kuongeza uelewa wake wakufikiri na kwenda kwa uhuru. Aliwaonea huruma wale ambao waliakataa na kuamua kujifungafunga mapangoni. Aliwaona waliojifunga wenyewe katika mtegeo wao wenyewe. Siku moja aliamua kurudi kwao na kuwaletea habari njema. Alifanikiwa kuwaeleza kile walichokuwa wanakikosa. Akatamani kuwafungua katika gereza lao.
Siiku moja akaamua kuchukua mwanga kwao kwakuchukua taa. Walipomuana na mwanga walikasirika wakamchukia wakampigia kelele wakamwambia ondoa mwanga hapa. Kelele zikazidi wakamrukia, wakamsukuma. Yeye alikuwa nabii wa kweli lakini akakataliwa na watu wake. Ni manabii wangapi sisi kama jamii, kanisa tumeshawakimbiza? Nabii sio lazima awe mtu mwenyewe mawazo fulani akipiga kelele kila mahali. Nabii ni yule ambaye yeye mwenyewe maisha yake ni ujumbe. Unaweza ukamchukia, ukamsingizia kila baya na hata kumuua lakini sauti yake hubaki ikiwa inazunguka. Mt. Teresa alikuwa ni nabii wa waliotengwa. Jean Vanier alikuwa ni nabii kwa waliovilema nk.
Yesu mwenyewe alikuwa nabii mkuu. Yeye ni neno kamili wa Mungu. Lakini kama ilivyo kwa nabii wa kweli alikataliwa na watu wake. Alitegemea kupata Imani ndani yao. Lakini aliwaambia kwamba alipata Imani zaidi kwa watu wa mataifa. Na kama ilivyokuwa kwa Mungu tangu zamani, upendeleo huu unaondoka kwao na kwenda kwa mataifa ambao wanaukaribisha. Walivyoshindwa kupokea hili walimfukuza katika kijiji chao, na kama wangeweza kumuua pia ingekuwa furaha yao.
Sisi kila mmoja wetu anashiriki unabii wa Kristo kwa njia ya ubatizo. Tuwe tayari kukubali kutoka katika giza la maisha yetu na kuigia kwenye mwanga. Tusiwatese au kuwakataa wale wanaotueleza ukweli wa maisha yetu. Tusijifungie Baraka wenyewe. Tuwapokee manabii na wala tusiwasingizie uongo kisa wanatuambia ukweli wa maisha yetu.
Sala:
Yesu tusaidie sisi tumpokee Yesu, huyu ambaye umempaka mafuta kuleta habari njema kwa maskini, uponyaji kwa walio na vidonda, mwanga kwa vipofu, na kutangaza kwa wote neema yako. Tunakuomba utufanye sisi tuweze kuwa manabii wa habari njema. Yesu nakuamini wewe.
Amina
Maoni
Ingia utoe maoni