Jumanne, Juni 28, 2016
Jumanne, Juni, 28, 2016,
Juma la 13 la Mwaka wa Kanisa
Kumbukumbu ya Mt. Ireneo, Askofu na Mfiadini
Amo 3: 1-8, 4:11-12;
Zab 5: 5-8;
Mt 8: 23-27
ALIPO YESU PANA UTULIVU!
Yesu alikemea upepo wa bahari na hali ikawa shwari. Kama sentensi hii inamaanisha kutuliza bahari tuu, mmoja anaweza kujiuliza swali, kwanini Yesu hafanyi sasa? Kwanini anaruhusu wapendwa wake wakumbwe na mawimbi makubwa ya maisha? Je, hayupo tayari kutuokoa kama alivyo waokoa mitume? Kuna mambo makubwa zaidi kutoka sentensi hii, ni zaida yakutuliza tu bahari. Sehemu yeyote alipo Yesu pana utulivu, upole na Amani. Haijalishi ni kwakiasi ghani maisha yanaweza kuwa mabaya na kukumbwa na mawimbi makubwa, uwepo wa Yesu tuu, unabadilisha hata kile tunachodhani hakiwezekana na hali ya utulivu hurudi tena. Tukiwa na Yesu katika boti yetu ya maisha hakuna mawimbi yatakayo tuangusha na kutupeleka mbali. Tatizo letu sisi tumekuwa watu wa Imani kidogo/hafifu. Imani yetu ni hafifu sana kiasi ambacho mambo yetu yasipoenda kama yalivyopangwa tunaanza kuwa na wasi wasi kuhusu uwepo wa Mungu ndani yetu. Ni kwa wale tuu waliojishika na Mungu na kuhisi uwepo wake ndani yao wanaosimama imara na kubaki vizuri bila kuyumbishwa. Watu hawa wanahisi Amani na utulivu katika hali zote, hata katika hali mbaya kabisa inayotisha katika maisha.
Mtakatifu Ireneo tunaye mwadhimisha leo, alipenda Amani na alitoa maisha yake yote kutetea Amani na kuhakikisha kanisa linabaki katika Amani kila wakati. Sisi tunapenda Amani? Sisi sio watu wa chanzo cha fujo na magomvi? Tunafurahi tunapoona watu wanaishi kwa Amani? Au tunatafuta mbinu za kuchafua Amani yao? je, unafanya jitihadi za kuleta Amani kati ya watu au maisha yako yamekuwa ya furaha kwasababu adui yako hana Amani au amepatwa na matatizo? Tunahimizwa ndugu zangu tuwe wajumbe wa kuleta furaha na Amani kati ya watu, tuache wivu usio na sababu, tujikubali wenyewe na tuwakubali ndugu zetu, tuwasamehe wakikosa, tuwe na moyo wakuomba msamaha tunapokosea, haya yote tukiyashika yatatufanya tuishi vizuri kwa Amani na furaha kati yetu. Tukiiishi kwa utulivu na Amani Yesu atakuwa kati yetu. Kwa maombezi ya Mt. Ireneo tuombe neema hiyo yakutunza Amani katika nafsi zetu, familia, ndugu wote na kanisa la Mungu.
Sala: Bwana, niongezee Imani na zamisha Imani yangu juu ya uwepo wako, ili niweze kuwa na utulivu mkubwa na Amani. Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni