Jumanne, Januari 08, 2019
[20:23, 1/7/2019] +255 783 250 049: Jumanne, Januari 8, 2019,
Juma baada ya Epifania.
1 Yoh 4: 7-10;
Zab 72: 1-4, 7-8;
Mk 6: 34-44.
KUTAMANI UTAKATIFU!
"Si kwamba sisi tulimpenda Mungu kwanza, bali Yeye alitupenda kwanza." Anaendelea kutujalia neema zake kwasababu ya huruma yake. Hata hivyo, watu wengi hawajitahidi kutafuta ukamilifu kama Watakatifu; huku wakifikiri kwamba sisi ni watu wa kawaida tu hatuwezi kufanya mambo makubwa kama wao. Kwa kweli, sisi hatujaribu hata kuwaiga kwasababu tunafikiri sisi ni watu dhaifu na wadogo mno. Kwa njia hii, sisi tunajifungia wenyewe kutopata neema ya Mungu, na hivyo kujifungia wenyewe kutohisi upendo wa Mungu kwetu. Injili anasimulia tukio la Yesu kulisha watu elfu tano kwa mikate mitano na samaki wawili tu. Yeye anaufurahisha umati mkubwa wa watu. Haya ndiyo anayofanya kila siku kwetu, Yesu anaendelea kutupa neema yake kila siku, ili mradi sisi tuitumie vizuri kukua katika utakatifu na wala Yesu haitaji kitu kingine kwetu zaidi ya sisi kuwa watakatifu.
Sala: Bwana, washa ndani yangu tamaa na bidii ya kutembea katika maisha ya utakatifu. Amina.
Copyright ©2013-2019 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
[21:39, 1/7/2019] +255 783 250 049: “ASALI MUBASHARA”
Januari 8, 2019.
------------------
Jumanne, baada ya Epifania
1 Yn 4: 7-10;
Zab 72: 1-4, 7-8;
Mk 6: 34-44.
KUTAMANI UTAKATIFU!
“Sio kwamba sisi tulimpenda Mungu kwanza, bali ni yeye alitupenda sisi kwanza” anaendelea kutupatia neema zake kila wakati. Lakini cha ajabu wengi wetu hatukazani kupata utakatifu na kuwa wakamilifu; kwasababu tunafikiri kwamba sisi ni dhaifu sana na hatuwezi kufanya mambo makubwa kama wao. Hata hivyo hatujengi ile tamaa ya kutaka kuwa kama watakatifu, tukidhani kwamba sisi ni dhaifu mno na hatuwezi. Kwa njia hii tunajifungia wenyewe neema za Mungu, na kujifunga wenyewe tusipate upendo wa Mungu wenyewe.
Somo la Injili linaeleza kuhusu Yesu kuwalisha watu elfu tano kwa kutumia mikatemitano na samaki wawili. Aliwalisha watu wengi na kuwafurahisha. Injili ya leo inatufunulia tena jambo jingine ambalo yeye haridhiki tu katika kutuponya na kutupatia vitu tu, bali leo alikuja na kujitoa yeye mwenyewe. Upendo unatuhitaji sisi tutoe pia kitu sio tu vitu bali hata muonekano wetu wa nje wakati tukiwa tunatoa vitu. Tendo hili la Yesu kutoa mkate lilikuwa likitangaza kuhusu kifo na ufuko wa Yesu. Yesu kujitoa mwenyewe kwetu kama mkate wa uzima, Ekaristi takatifu.
Sisi kama Yesu tunapaswa kuwa mkate kwa wengine. Somo la kwanza Yohane anatuambia kwamba upendo wa kweli haupimwi kwa dini au kwakushika dini au kwa akili bali katika kumpenda jirani. Ni vizuri kutambua kwamba Yohane ameanza kwakusema kwamba “ndugu zangu wapendwa tupendane, kwasababu pendo latoka kwa Mungu”. Hii ina maana kwamba hatuwezi kupenda mtu kama hatujapokea upendo wa Mungu kwanza. Bila kuwa na ufahamu wa Mungu na kuupata upendo wa Mungu, swala lakumpenda jirani ni ngumu sana. Bila upendo wa Mungu hatuwezi kupenda. Bila nguvu ya upendo hatuwezi kuwa na ukarimu kati ya watu.
Hivyo sasa upendo huu wa Mungu unapatikana wapi? Ukweli ni kwamba ndani ya Yesu! Kwetu sisi Noeli na Epifania sio tukio la kizamani. Kwetu sisi wakatoliki kila tunapoadhimisha Misa Takatifu, mkate hugeuga kuwa mwili wa Kristo na divai kuwa damu yake. Kwakumpokea Yesu, tunapata nguvu ya kuwa mkate wa ulimwengu. Hata hivyo kanisa linatualika kutafakari juu ya kumpokea Yesu na yeye kuja katika maisha yetu kwa njia ya Ekaristi na wakati pia tunapokutana na watu kwa upendo na huruma.
Sala:
Bwana, Wakati mwingine ninakuwa na wasi wasi na neema zako na uwepo wako katika maisha yangu. Nijaliye niweze kukufuata katika mwaliko wako huu wenye huruma. Nisaidie niongozwe nawe siku zote ili niweze kuishi daima kadiri ya mapenzi yako.
Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni