Ruka hadi maudhui
Mkatoliki Leo
Tafakari

Tafakari ya Jumatatu, 7 Januari 2019

· na Shajara Administrator

Masomo ya siku hii Jumatatu baada ya Epifania → 1Yoh. 3:22-4:6 · Zab. 2:7-8, 10-11 · Mt. 4:12-17, 23-25
Jumatatu, Januari 7, 2019,
Juma baada ya Epifania

1 Yoh 3: 22-24; 4: 1-6;
Zab 2: 7-8, 10-118;
Mt 4: 12-17, 23-25.


Yesu hakuwa mhubiri peke yake, alikuwa akihubiri kile alicho ishi. Alihubiri Ufalme wa Mungu. Mafundisho ya Yesu yaliamsha mawazo ya kibinadamu. Mienendo ya Yesu, na miujiza yake ilikuwa ni habari njema kwa Maskini. "Injili" ilikuwa uwepo wa Yesu mwenyewe, furaha na ushirika uliokuja kwaajili ya maskini. Hivyo 'Ufalme wa Mungu' Yesu aliohubiri si 'kitu' bali ni 'mtu' - mtu ambaye ni uwepo wake Yesu mwenyewe.

Yesu amepita juu ya Ufalme huu kwamba yeye anautambulisha kwa wale wote wanaotubu na kumwamini. Sisi pia, ni watoto wa Mungu, anatufanya warithi wa ufalme huu.

Sala:
Bwana, tufanye sisi tuwe tayari kupokea Ufalme wako.
Amina.
0 Maoni

Maoni (0)

Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.

Ingia utoe maoni