Jumatatu, Disemba 31, 2018
Decemba 31, 2018.
------------------------------------------------
JUMATATU, OKTAVA YA KRISMASI
Somo 1:1Yn 2: 18-21 Yohane anakataza kwa ukali kabisa kuhusu wapinga Kristo ambao wamekataa kumuelewa Kristo na wanawafanya wengine waende mbali kutoka katika ukweli.
Wimbo wa Katikati: Zab 95: 1-2, 11-13, Mbingu zifurahi na nchi ishangilie.
Injili: Yn 1: 1-18 , Tunasikia tena kuhusu maneno ya Yohane ya mwanzo wa Injili yake kuhusu Neno wa Mungu akatwaa mwili , nasi tumeuona utukufu wake.
------------------------------------------------
FUMBO LA NENO
Injili ya Yohane inatufunulia fumbo kuhusu Neno, neno ambaye ni wa milele anachukua mwili, yeye ambaye tangu asili ni Mungu. Huyu neno ni Yesu. Tunafunuliwa kwamba Mungu aliongea kwa neno wake na kufunua mpango wake uliokamili kwa njia ya neno huyu, yeye ambaye ni Mwana wa Mungu. Kwa njia hii ya kuishi na Kristo na kumuona, Yohane alitambua kwamba Yesu alikuwa Neno ambaye ni Mungu na aliishi na Mungu tangu awali. Yeye sasa amechukua mwili Akakaa kwetu. Na hili linatupatia ufupisho wa maisha yote ya Imani ya ukristo. Ukristo sio dini ya kitabu bali ni dini ya neno la Mungu, sio kwa maneno yalioandikwa na kuachwa bali ni neno lililo mwilishwa.
Kwa hiyo katika Ekaristi takatifu wakati habari njema inahubiriwa kwa namna ya pekee, ni Yesu mwenyewe anajitangaza kwa njia ya wapakwa mafuta wake,akiwatafuta wale ambao watajibu kwa njia ya Imani na upendo. Na Kanisa katika kiini chake hujikita kwa wale wanaolisikia neno lake na kulipokea. Swali ni kwamba wewe kama mmoja wapo wa wale wanaosikiliza neno hili huwa unajibu je? Unalifanyia kazi? Je tunalifanyia hili neno kiburi na kulikataa lisitubadilishe? Tunakataa neema yake?
Sala:
Bwana Yesu, Neno wa milele wa Baba,tunakushukuru kwa kuja kwetu na kuamua kukaa nasi. Tunakushukuru kwa mafumbo makubwa ya Noeli. Nisaidie mimi daima nisheherekee kipindi hiki kwa furaha na shukrani. Ninakuomba mafumbo haya yanisogeze kwako daima kwa mapendo zaidi. Yesu nakuamini wewe.
Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni