Jumatatu. 16 Septemba. 2024

Tafakari

Jumamosi, Oktoba 01, 2016

Jumamosi, Oktoba 1, 2016.
Juma la 26 la Mwaka


Kumbukumbu ya Mt. Theresia wa Mtoto Yesu, Bikira na Mwalimu wa Kanisa.

Ayu 42: 1-3, 5-6, 12-17
Zab 118: 66, 71, 75, 91, 125, 130
Lk 10: 17-24

MUNGU WA VITU VIDOGO!

Somo la kwanza leo linatueleza ni kwa jinsi ghani Mungu alivyo zibariki siku za mwisho za Ayubu zaidi hata ya zile za mwanzo. Na Ayubu aliamini kwamba Mungu anaweza kutenda na kutoa vitu vyote kwa mwanadamu na kwamba hakuna lengo lake linalo weza kuzuiwa na kitu chochote au nguvu za muovu.

Wale sabini wanavyorudi wakielezea ushindi, kuna aina tatu za furaha katika Injili ya leo:
1) Furaha ya huduma
2) Furaha ya ukombozi
3) Furaha ya mamlaka.

Yesu aliwapa nguvu na uwezo wakuponya na kutoa pepo wabaya, na kuhubiri Neno, na hatimaye walishinda. Kila ushindi ni muhimu kwa Yesu, haijalishi ni namna ghani waweza kuonekana machoni petu. Lakini, Wafuasi hawapaswi kufurahi kwasababu pepo wabaya wana watii na kuwatoka watu bali kwasababu majina yao yameandikwa mbinguni. Furaha au ushindi waweza kumfanya mtu kuishia kujivuna. Muujiza mkubwa kuliko wote ni ukombozi wa roho iliyo potea. Furaha yetu haipatikani katika huduma, na wala si katika ukombozi, bali ni katika kujikabidhi kwenye mapenzi ya Baba Yetu wa Mbinguni, kwawasababu hii ndio sababu ya huduma na ukombozi.

Leo Kanisa lina adhimisha kumbukumbu ya Mt. Teresa wa Mtoto Yesu, anaye elezewa kama mtakatifu mkuu wa kipindi cha sasa, huyu Bikira mdogo anaelezewa pia kama msimamizi wa utume. Huu ndio mchango wake na msukumu wa maisha yeke kwa ufupi. Kanisa likimtangaza kama ‘Mwalimu wa Kanisa’ linatambua mchango wake, tena mafundisho yake ya kawaida, ‘Njia ndogo”, kinachojulikana kama ‘Roho ya utoto’. Mafundisho yake yamejikita katika mafundisho na msingi wa maneno ya Yesu “Aliye mdogo na aje kwangu”. Na hivyo, Mt. Teresa hakuelewa tu siri hii kubwa katika unyenyekevu, kumwamini Mungu na kuwa wazi kwake, kujiamini na bila kumwacha, bali pia alitumia ngazi hii kukwea katika mlima wa ukamilifu na utakatifu na kuungana na Mungu. Teresa anatukumbusha kwamba, kiini cha ujumbe wa Mkristo ni kwamba, Mungu ni upendo, yeye ni Baba wa huruma, na anajitoa mwenyewe kwa wale wote walio maskini wa roho kwa ajili ya neno la Mungu. Ni nani kati yetu anaye shindwa kumtukuza Mungu kwa njia hii rahisi ya kumfurahisha Mungu na kukuwa katika utakatifu?

Sala: Ee Bwana, tuongoze kwenye njia ya udogo na unyofu wa Moyo. Amina

Maoni


Ingia utoe maoni