Jumatatu, Novemba 12, 2018
Jumatatu, Novemba 12, 2018,
Juma la 32 la Mwaka wa Kanisa
Tit 1:1-9
Zab 23:1-6
Lk 17:1-6
SOMO LA MAISHA YA UFUASI
Kuna sheria tatu katika sehemu ya Injili leo. Zinaweza kuleta mabadiliko katika maisha ya muumini. Atakayefuata sheria hizi kikamilifu atafanya mabadiliko katika maisha yake.
Sheria hizi ni:
1.Dhambi haitabiriki kama Yesu alivyosema ‘makwazo hayana budi kuja’ kwa namna nyingine nisawa nakusema, vitu vinavyo sababisha dhambi havina budi kuja. Lakini kuwaongoza wengine kwenye dhambi ni kitu kibaya kabisa.
2. Yesu alisema kwamba, kama mtu akikukosea umuonye, lakini akiomba msamaha, umsamehe, haijalishi ni dhambi kubwa kiasi ghani, haijalishi ni jiwe kubwa kiasi ghani aliloweka katika njia zetu
.
3. Imani ni ufunguo wa nguvu zote ulimwenguni. Mfuasi anapaswa kuwa na Imani sahihi. Msisitizo si juu ya Imani kiasi ghani alionayo mtu, ni kitendo tu cha kuwa na Imani na kuishi nayo.
Yesu katika hali ya mfano anaongelea kuhusu kungoa mti nakuutupa baharini. Wakati tunapo patwa na mambo ambayo hayawezekani katika maisha yetu, tunapaswa kutumaini nguvu ya Mungu ili tuweze kufanya yasiowezekana.
Sala:
Bwana, ongeza Imani yetu ili tuweze kujenga ufalme wako.
Amina
Maoni
Ingia utoe maoni