Jumatano. 27 Novemba. 2024

Tafakari

Jumamosi, Novemba 10, 2018

Jumamosi, Novemba 10, 2018,
Juma la 31 la Mwaka wa Kanisa

Fpl 4:10-19;
Zab 111:1-2, 5-6, 8-9;
Lk 16:9-15

KIZAZI CHENYE KUWAJIBIKA.
Kutambulishwa na kukuwa kwa teknologia imeleta msaada mkubwa sana katika maisha yetu ya kila siku, lakini kwa upande mwingine ni kama imetukata mikono. Tunaona watu wengi muda mwingi wakiwa na simu zao, tableti na kompyuta wakiangalia facebook, meseji za whatsapp, Twitta nk. Tunaona watu wanashugulika zaidi na simu kuliko watu walionao karibu. Mbaya zaidi wengine wakichati hata wakati ule wakula kwenye familia, au hata wakiwa wamealikwa kwenye sherehe watu hawaongei tena, wako bize na sumu zao. Mikono yetu imekatwa na teknologia hatuwezi tena kusaidia wengine, na wala hatuna tena muda wakuongea kijumuiya. Tumetekwa kifikra na kiakili hatuweze kuongea na wenzetu walio karibu nasi, tukiulizwa swali tunasema tuu ndio au hapana na wala hatujui kwanini tumesema hivyo, kwasababu akili na mawazo yetu hayapo pamoja na wengine walio karibu. Tunaishia kwenye ubinafsi. Kuhusu hili limewashika wengi na ni vizuri kujichunguza, tunapoteza ile furaha na upendo wa kuongea na ndugu walio karibu nasi.

Ni dhahiri kwamba, tuna tabia ya kutupa ya zamani na kutaka mapya. Nguo mpya, simu mpya, magari mapya nk. Sasa tunataka kutupa tamaduni zetu njema na kuiga tamaduni zinazo haribu asili yetu kama wanadamu. Tunadharau hata tamaduni zetu zenye maadili mema tukidhani mambo mapya ndiyo yenye maana.
Masomo ya leo yanatualika tuwe mawakili waaminifu katika kutumia vitu vyetu tulivyonavyo. Je, vitu vyetu vinatuweka karibu na Mungu au ndio vinafuta hata kile kidogo nilichonacho? Tumetumia vipaji, zawadi na mali zetu na wengine? Je tumekuwa watumwa wa vitu tulivyo navyo? Hatuna wasi wasi kwamba mali tulionayo ni Baraka kutoka kwa Mungu kama tumeyapata kwa haki na maadili mema. Kwanza kabisa kama Wakristo, tunapaswa kutumia vyote tulivyo navyo kwa faida ya wengine. Pili, kama mmoja akiwa mwaminifu katika kushirikisha ya duniani, Mungu pia atamshirikisha utajiri wa Mbinguni. Na tatu, tutambue utajiri wa duniani una thamani ya duniani.

Paulo anakiri kwamba, Wafilipi wamekuwa Kanisa pekee lililokuwa na ukarimu kwa mali zao wakati akiwa gerezani, akipata mateso. Walimpatia msaada kila mara. Na zaidi sana, ilikuwa ni sadaka safi yenye kumpendeza Bwana. Je, waliitikia vipi kuhusu mahitaji ya Paulo akiwa gerezani? Walikusanya mchango kwa upendo na kumpa Epafra, ampelekee Paulo mahitaji. Na mwisho kabisa walilisaidia kanisa na kutumia utajiri wao kwa ajili ya wengine.

Sala:
Bwana, nisaidie mimi niweze kuwa muwajibikaji wa kushirikisha nilivyo navyo utajiri wa mali na utajiri wa kiroho.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni