Jumatano, Novemba 07, 2018
Jumatano, Novemba 7, 2018.
Juma la 31 la Mwaka
Flp: 2:12-18;
Zab 27: 1.4.13-14,
Lk 14: 25-33.
GHARAMA YA KUWA MFUASI!
Katika injili ya Luka, tunaona Yesu yupo njiani kuelekea Yerusalemu. Ndani ya akili yake akiwa amejaa na kuhusu mateso, kifo na ufufuko ambavyo vingempata. Umati ulikuwa ukitembea pamoja naye lakini katika ukweli ulikuwa hautembei naye. Umati ulikuwa ukidhani kwamba Yesu amekuja kuwakomboa kutoka katika magonjwa, upungufu wa fedha na utawala wa Kirumi. Yesu anawakumbusha umati kitu ambacho kinahitajika ili waweze kutembea naye katika hali ya ukweli na mafanikio. Anawaambia kwamba ufuasi sio kazi rahisi ya kuomba. Kumfuata yeye inampasa mmoja kuacha ndugu hata wa familia na kumfuata, baba, mama, mwenzi wa ndoa, watoto nk. Kwa maneno mengine kumfuata Yesu tunapaswa tumuweke wa kwanza zaidi ya kitu kingine.
Yesu anaelezea mambo matatu katika ufuasi: kuachana na kujishika na familia, kukutana na kujikatalia binafsi na kuachia mali. Anawaalika wale wote ambao watamfuata yeye waweze kukubali na kutopata heshima na kupata mateso. Mfuasi kamili wa Yesu hatafuti faraja, kufarijiwa na marafiki, wala kubakiza maisha yake. Hivyo ufuasi sio rahisi, kuna gharama isio isha. Je, mimi na wewe tupo tayari kulipa gharama hiyo?
Sala:
Bwana Yesu, nisaidie niweze kuona vile vitu vyote vinavyo nizuia mimi nishindwe kukupenda wewe. Nikiwa ninatambua kitu ambacho kinanitoa kwenye Imani, nipe ujasiri niweze kukuchagua wewe zaidi ya kitu kingine. Nipe hekima niweze kutambua ni kwa jinsi ghani naweza kukuchagua wewe zaidi ya kitu chochote. Yesu, nakuamini wewe.
Amina
Maoni
Ingia utoe maoni