Jumatano. 04 Desemba. 2024

Tafakari

Jumamosi, Septemba 24, 2016

Jumamosi, Septemba 24, 2016.
Juma la 25 la Mwaka


Mhu 11: 9 - 12: 8
Zab 89: 3-6, 14, 17
Lk 9: 43-45


UBATILI: MAISHA BILA MUNGU!

“Ubatili mtupu; mambo yote ni ubatili, Mhubiri asema!” (Muh 12: 8). Kitu ambacho Mwandishi anakiita ubatili ni maisha bila hofu ya Mungu. Maisha ya kufurahia maisha na zawadi zote tulizo pewa bila kujali nafasi ya mwenzangu (jirani) ambapo mtu anakuwa kipofu kuhusu mahitaji ya wengine. Lakini maisha anayoishi mtu kwa ajili ya Mungu na kwa ajili ya watu wake, yanakubalika sana na yana matunda mengi.

Yesu leo katika somo la Injili anaongelea kuhusu kifo chake. Lakini mitume hawakuelewa fumbo hili kuu. Yesu alimpenda Baba yake sana kiasi kwamba alikuwa akijiandaa kutimiza mapenzi yake. Nasi ndicho tunachopaswa kufanya, tunapaswa tujitahidi kuyajua mapenzi ya Mungu kwetu na kujaribu kuyatimiza katika maisha yetu. Na hapo maisha yetu hayatakuwa maisha ya ubatili.

Sala: Bwana mpendwa, tubariki wote na tuongoze ili tuweze kutambua mapenzi yako kwetu ili tuweze kuongozwa na maisha ya fadhila. Amina

Maoni


Ingia utoe maoni