Jumatatu, Oktoba 01, 2018
Jumatatu, Oktoba 1, 2018,
Juma la 26 la Mwaka wa Kanisa
Kumbukumbu ya Mt. Teresia wa Mtoto Yesu
Ayu 1:6-22
Zab 17:1-3.6-7
Lk 9: 46-50
KUJITEGEMEZA KWA MUNGU BABA YETU!
Leo Injili inaanza na majadiliano kati ya wanafunzi wa Yesu juu ya nani aliye mkubwa. Yesu alikuwa amemaliza kuwaambia wanafunzi atakapo ingia Yerusalemu, atatiwa mikononi mwa wakuu na watawala na kwamba atauwawa. Ana wafumbulia kwamba bado kidogo atayapoteza maisha yake na wao madai yao wanajiuliza ni nani wa kwanza kati yao!.
Yesu anajibu jambo lao kwakumchukua mtoto mdogo na kumweka karibu yake. “Anaye mpokea mtoto mdogo kama huyu kwa jina langu amenipokea mimi…kwasababu aliye mdogo kati yenu ndiye aliye mkubwa”. Katika utamaduni wa kipindi cha Yesu, mtoto aliwakilisha “mdogo kabisa” kwasababu hawakuwa na chochote cha kumpa mtu. Utu wao ulikuwa ni kwasababu wapo tu, na sio kwasababu walikuwa na nguvu fulani au umaarufu fulani.
Wakati tunapokuwa kuelekea utu uzima, mara nyingi, ni rahisi kudhani tunakuwa tunapunguza kuwa tegemezi na kuwa tayari zaidi kujitegemeza wenyewe. Yesu anatukumbusha kwamba, sivyo, ambapo ni vigumu kwa mtu kama sisi ambao tunafikiri sisi tunaji tosheleza na tunaweza kujijali na kupambana na mambo sisi wenyewe. Walio wakubwa ni wale wanao tambua wanahitahi wengine, wanao jiruhusu kuhusiana na wengine, kwasababu ni watu hao wanaotenda yaliyo katika asili ya Mungu na wanatambua asili yao wenyewe inategemezwa na Mungu. Tunapo jinyenyekesha na kukubali utegemezi wetu kwa Mungu na wengine, na kukubali udhaifu wetu na kuto kukamilika kwetu, ni vigumu kuwatenga wengine na kuwa hukumu wale ambao ni tofauti na sisi na wale wasio ishi kadiri ya sisi tunavyotaka. Tukianza kutembea katika njia hii, tutatambua kuwa tumenza kuwa wakubwa mbele ya macho ya Mungu.
Tumtegee Mungu daima kama Ayubu kama tutakavyosikia kutoka katika somo la kwanza. Ayubu alitambua kuwa Mungu ndiye tegemezi kwake licha ya mabaya tena makubwa na majaribu mengi yaliompata. Yeye alisimama imara na alijua nguvu zake zina tegemezwa na Mungu.
Sala:
Bwana, tusaidie tuweze kutambua kwamba WEWE ni kielelezo, na kwamba ni wewe tunakutegemea kila wakati. Bwana naomba nisiwe tegemezi-binafsi bali niwe Yesu-ananitegemeza.
Amina
Maoni
Ingia utoe maoni