Ijumaa, Septemba 28, 2018
Ijumaa, Septemba 28, 2018,
Juma la 25 la Mwaka wa Kanisa
Muh 3: 1-11
Zab 143: 1-4
Lk 9: 18-22
KRISTO NI NANI KWANGU?
Katika Injili tunamuona Yesu akiwauliza wanafunzi wake maswali mawili. “watu wanasema mimi ni nani? na “nyie mnasema mimi ni nani?” Yeye mwenyewe alijitambua ni nani. Kwahiyo, Yesu anauliza maswali kama mpango wake wakuendelea kujifunua kwa wanafunzi. Alitaka wanafunzi wake wamtambue yeye, ametoka wapi na kwanini amekuja. Swali la Yesu pekee lili hitaji jibu la mtu binafsi kutoka kwa Wanafunzi wake. Hata sisi leo Yesu ana tuuliza swali hilo hilo: ‘wewe unasema Yesu ni nani?’
Katika somo la kwanza muhubiri anatueleza kwamba kuna muda wa kila kitu. Pamoja na muda wote ambao tunaoweza kuwa nao hakuna muda ulio na maana zaidi ya muda ule wa Bwana. Muda huu ni wa maana kwani unatujengea hazina ya baadae. Tuangalie vizuri katika kumpatia Bwana muda wake. Tusiwe wachoyo wa muda wa sala au muda wa misa kwani muda huu ni wa muhimu zaidi kwani ndipo tunapokutana na Bwana na kutengeneza maisha yetu yajayo ambayo ni ya muhimu kuliko maisha ya sasa. Biashara, shule yako, kazi yako isiibe muda wa Mungu. Ni katika muda wa Bwana tunaweza kujibu swali la Yesu kwamba yeye ni nani? Petro aliweza kujibu kwasababu alikuwa karibu na Bwana. Je, wewe unaweza kumfahamu Bwana ni nani wakati huna muda wa kukaa naye? Kaa na Bwana ili akija kukuuliza mimi ni nani uweze kusema vizuri bila kusitasita.
Sala:
Bwana, nisaidie niweze kukufahamu wewe kwa karibu kabisa na kukuamini.
Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni