Jumatano. 27 Novemba. 2024

Tafakari

Alhamisi, Septemba 20, 2018

Alhamisi, Septemba 20, 2018,
Juma la 20 la Mwaka

Kumbukumbu ya Mt. Andrea Kim na wenzake mashahidi.
1Kor 15:1-11
Zab 117: 1-2, 15-17, 28;
Lk7: 36-50.


KUOMBA HURUMA
Somo la Injili linatuambia kuhusu Farisayo mmoja aliye mwalika Yesu kwa mlo. Baada ya Yesu kuingi katika nyumba ya Farisayo anakuja mama mmoja mwenye dhambi na kuja na mafuta na kumpaka miguuni huku akilia na kupangusa miguu ya Yesu kwa nyewele zake na kuibusu miguu yake na kuipaka mafuta. Mafarisayo wanatoa hukumu kwa huyu Mama pamoja na Yesu. Yesu anamrekebisha kama alivyofanya kwa Mafarisyo wengi.
Mama huyu anaonesha mapendo kwa Yesu na moyo uliojaa huzuni kuhusu dhambi na kuwa na unyenyekevu. Dhambi yake ilikuwa kubwa na kwa matokeo yake lakini pia unyenyekevu wake na upendo wake ulikuwa mkubwa pia. Unaonekana katika matendo yake kama alivyokuja kwa Yesu.

Kwanza, “alisimama nyuma ya Yesu…”
Pili, alianguka chini miguuni pa Yesu…”
Tatu, alikuwa akilia…”
Aliosha miguu yake kwa machozi yake…”
Tano, alikausha miguu ya Yesu kwa nywele zake…”
Sita, alibusu miguu yake.
Saba, aliipaka miguu yake mafuta ya bei ya juu.

Kama tukio hili sio tukio la majuto makuu, toba na unyenyekevu basi itakuwa ni vigumu kujaribu kuelewa nikitu gani tofauti. Ni unyoofu wa hali ya juu na kwa njia hii aligusa huruma ya Yesu bila hata kusema neno lolote.

Tafakari leo juu ya dhambi zako mwenyewe. Usipo itambua dhambi yako huwezi kuwa na unyenyekevu na toba hii ya namna hii. Je, unatambua dhambi yako? Kuanzia pale anza kufikiria jinsi ya kuanguka magotini pa Yesu nakuomba huruma yake. Jitahidi kulifanya hilo na Yesu atakufanyia yale yale aliomfanyia yule mwananmke.

Sala:
Bwana, ninaomba huruma yako. Mimi ni mdhambi na nastahili adhabu. Ninakiri dhambi zangu. Ninakuomba unisamehe dhambi zangu na unipe huruma yako juu yangu. Yesu nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni