Jumatano. 27 Novemba. 2024

Tafakari

Jumapili, Septemba 16, 2018

Jumapili, Septemba 16, 2018.

Juma la 24 la Mwaka wa Kanisa

Isa 35: 4-7;
Zab 146: 7-10;
Yak 2: 1-5;
Mk 7: 31-37.


KUWA MKWELI KWA NAFSI YAKO
G. K. Chesterton anatueleza habari ya mtu mmoja ambaye alikuwa akipendwa sana na alikuwa akiwahudumia wengi. Alikuwa maarufu sana na watu wengi walimfahamu na alikuwa akiwahudumia watu na hasa kuwapatia ushauri wa maisha hasa pale mahali ambapo maisha yalionekana kwenda vibaya. Yeye alikuwa daima akionesha uso wa tabasamu. Na watu walimuona kuwa mtu wa namna yake kuzaliwa. Alikuwa akicheka daima na kuonesha furaha.

Lakini cha ajabu siku moja huyu mtu alikutwa akiwa amekufa katika mazingira ya kutatanisha. Wakafanya uchunguzi mkali na kutambua kwamba mtu huyu alikufa kwa kujinyonga. Watu walikataa kusikia habari hizo na kusema haiwezekana mtu kama yule ambaye alikuwa akionekana akiwa anacheka daima ajinyonge, kwani alikuwa na shida gani? Lakini ukweli ni kwamba alijinyonga. Lakini ukweli ulifunuka taratibu kwamba alikuwa ni mtu aliyekuwa na mambo mengi moyoni mwake na hakupenda hata kidogo kushirikisha na aliumia mwenyewe moyoni ingawaje alijaribu kuonesha furaha kwa wengine. Kwasababu ya watu wengi kumtegemea mno aliona isingekuwa safi aoneshe udhaifu mbele zao na kujifanya.


Hii ni hali ya juu lakini inatueleza jambo Fulani katika maisha yetu ya kila siku. Kila mtu anapenda kujulikana. Na watu wanapenda wajulikane machoni pa watu, hujitahidi kutenda mema machoni pa watu na kuonesha sura njema ili kujenga jina. Watu hawa huhitaji kusifiwa mnoo na kushangiliwa. Wanapapata changamoto au kikosolewa huumia sana kwani huona kana kwamba anapoteza jina lake. Hawawezi kusema au kushirikisha madhaifu yao kwa mtu kwani hawapo tayari kuonesha udhaifu.

Tukiangalia katika somo la Injili tunaweza kugundua ni kwa jinsi gani Yesu hakujali sana yale mambo ambayo watu walikuwa wakimwazia. Ingawaje walikuwa na mawazo ambayo sio sahihi. Walikuwa na mawazo mbali mbali kuhusu yeye ni nani. Wengine walidhani kwamba yeye ni Yohane Mbatizaji amekuja tena.Wengine walidhani kwamba yeye ni Elia wa Agano la Kale au mmoja wa manabii wa Agano la Kale. Ni Petro mwenyewe aliyetambua Yesu ni nani kwamba ni Masiha. Ingawaje hakujua vizuri sana. Petro pia aliamini maneno yaliokuwa yanasemwa kuhusu Masiha mpya kwamba atakuwa mtu wa vita na atakuwa kama Daudi mpya, ambaye ataanzisha Isareli mpya kwa kutumia nguvu za kijeshi. Lakini Yesu hakuwa na lengo lakuishi na kufuata usemi wa watu wengi. Angefanya hivyo hakuna shaka kwamba angekuwa na watu wengi mnoo na ni wazi kwamba angepata umaarufu mnoo kwa watu na kusifiwa. Lakini ni wazi kwamba asingekuwa na ukweli wa moyo wake kwamba ametumwa na Baba yake ili kutimizia mapenzi yake.

Kila mmoja anaweza kuvutwa na akili ya Yesu ya Pekee. Hakuna hata mmoja ambaye angeweza kubadilisha lengo hili la Yesu. Sio wale watu wala Petro aliyejaribu kumshauri tofauti. Alikuwa mkweli kwa nafsi yake na Baba yake. Hapa alikufa kwa nafsi yake ya njee ambayo hujengwa na watu kwa sifa za uongo. Lakini inaleta pia maisha ya kweli ya kuishi ukweli wa moyo kwa kufanya kile ambacho kinapaswa kutendwa.

Watu wengi katika maisha haya huvaa maski. Lakini kitu kimoja tu ambacho tunahakika nacho, nacho ni hatuwezi kuingia katika ufalme wa Mungu tukiwa tumevaa maski. “kabla hawajafa watu waliovaa maski, watalia na kusema kwanini sikuishi vizuri kwa ukweli na bila maski” kwanini nilificha ambacho hakipaswi kufichwa? Ukweli wa maisha yangu.

Katika uhalisia, ukweli wa maisha kinachohitajika ni kuishi ukweli wa maisha yetu. Aina nyingine ya maisha haiwezi kuwa na furaha wala kukuwa. Baada ya kifo tutaingia katika ukweli wa maisha. Na hapo tutakuwa kama tulivyo kuliko kuishi katika maisha na kujifanya kuishi maisha ambayo sio yako. Lakini hatupaswi kujificha mpaka wakati huo.

Sala:
Baba, chanzo cha kila kilicho chema, unatambua udhaifu wetu. Tunakuomba tukimbilie ukweli wako na kuuelewa na kuufuata. Yesu nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni