Jumapili, Agosti 19, 2018
Jumapili, Agosti 19, 2018.
Dominika ya 20 ya Mwaka Wa Kanisa
Mit 9: 1-6;
Zab 33: 2-3, 10-15;
EF 5: 15-20;
Yn 6: 51-58.
EKARISTI: KARAMU YA KIMUNGU
Jaribu kujifanya kana kwamba umealikwa kwenye mwaliko wa ufumbuzi wa shule mpya. Na wewe ni mzazi mwenye mtoto katika shule hiyo. Watu wengi kama mia moja hivi wamekusanyika katika bwalo la shule. Kuna viti maalumu vilivyo hifadhiwa kwa ajili ya watu maalumu na mgeni rasmi. Pengine mmbunge flani au waziri flani amealikwa kujakufanya ufunguzi wa hiyo shule. Kuna maada mbali mbali na hivyo sasa muda umefika wa kufungua tukio lenyewe. Kuna kuwa na makofi na vigelegele alafu Mgeni rasmi anaingia na tena wanamchukua sehemu tofauti iliyo andaliwa na hapo wewe pamoja na wengine mliokuja ndio mwisho wa sherehe. Mgeni rasmi anaenda sehemu maalumu ambapo huku sherehe itaendelea. Wewe pamoja na wachache mnaachwa. Na hapo kumbuka mtangazajI ameshakusifia kwamba hii ni shule yenu. Ni yenu katika hali ya kwamba bila watoto wenu isingekuwa shule. Alafu unasikia vigelegele na nderemo nyingi ndani alipoingia mgeni rasmi. Unasikia vinywaji vikinyweka na kugonganisha glasi lakini wewe huruhusiwi kuingia. Wewe ulikuwa na nafasi yako ya kusikiliza maada tu na baada ya hapo huna nafasi ya kuingia ndani. Wewe ni wa kunusa harufu ya chipsi na nyama. Hakuna hata mmoja anayekuja ili kukukaribisha wakati wewe ulijiona ni mtu wa maana pale.
Leo tunasheherekea karumu ambayo Bwana amewaachia wafuasi wake, karamu ambayo inapaswa kuwafanya hai na kuleta umoja. Katika karamu hii Yesu mwenyewe anakuwa ndiye mkate wenyewe. Sehemu ya kwanza ya karamu hii kuna maada mbali mbali (masomo na homilia). Hii ni sehemu muhimu kabisa na inapaswa kuchukuliwa kwa makini. Ingawaje katika uhalisia tunakuwa tunajiandaa. Lakini kiini cha karamu bado hakijaja (liturjia ya Ekaristi Takatifu), tunatakiwa kuula mwili na kunywa damu ya Kristo ili sisi tuweze kushiriki katika kitu ambacho yeye mwenyewe amekiita “mkate wa uzima”.
Tofauti na sherehe ya shuleni hapa tunaalikwa wote. “twaeni mle..twaeni mnywe”. Na Hapa ni Yesu mwenyewe anayetualika. Hakuna hata mmoja anayetengwa. Lakini kunatokea nini? Kwa uhuru wetu sisi wenyewe tumeamua tusishiriki. Ni ajabu watu wasiompokea wanajiona wana sababu nzuri za kuacha kumpokea. Pengine wanajiona hawastahili. Na jibu kwa hili ni kwamba hakuna anayestahili. Tunampokea wote kwasababu Kristo ametualika, na ukweli kwamba hatuwezi kuishi vizuri bila kula chakula anachotupatia Kristo.
Mama Teresa anasema: “Katika Ekaristi napokea chakula cha Kiroho kinacho nitia nguvu katika kazi zangu. Bila hicho nisingeweza kufanya kazi hata moja katika siku zangu za kuishi”. Tunaweza kujisikia kwamba tupo katika dhambi. Kama ndio hivyo basi kuna sakaramenti nyingine (sakaramenti ya Kitubio) ambapo naweza kukutana na masamaha wa Yesu na kurekebisha hayo. Na kwa zile ambazo zinaitwa dhambi nyepesi ambapo hata katika Biblia tunaambiwa kwamba hata mtu mkamilifu huanguka katika hizi mara nyingi katika siku, tunapata nafasi ya kuziungama kabla ya misa. Na hivyo hazipaswi kutufanya sisi tushindwe kumpokea Yesu. Yasikilize tena maneno ya Kristo ya uzima wa milele. “anayekula mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele”. Ni ahadi iliyoje? Je, napaswa kuishi bila kuistahili kweli? Yesu ambaye anajifanya kwangu kuwa kama ndugu.Yupo anakuja kwangu kana kwamba nipo pekee yangu ulimwenguni, anayestahili kwake. Anakuja kwangu kwasababu ananipenda na mimi ni wa thamani kwake.
Sala:
Bwana, nisaidie mimi niweze kuwa jasiri kwako. Nisaidie mimi niweze kukusikia ukiongea nami katika sikio langu kwa ukweli na mapendo. Katika matendo na hali ya kutokuelewa naomba ulete neno lako linifanye mpya. Nisaidie mimi niweze kukutamani katika Ekaristi Takatifu. Ninakuomba niweze kupambwa na upendo mkuu kwako unaotoka katika zawadi hii yako Takatifu. Yesu anakuamini wewe.
Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni