Jumatano, Agosti 08, 2018
Jumatano, Agosti 8, 2018,
Juma la 18 la Mwaka wa Kanisa
Kumbukumbu ya Mt. Dominiko
Yer 31: 1-7;
Yer 31: 10-13;
Mt 15: 21-28
WOTE NI WATOTO WA MUNGU!
Mwanamke Mkanaani katika Injili anakuwa kielelezo cha Imani. Ni mmoja wa wana Wakanaani, maadui wakubwa wa Waisraeli katika Biblia ambao kwa upagani wao waliwasababisha Waisraeli wamuache Mungu na kuabudu miungu ya uongo.
Yesu hamlaani mwanamke bali anajaribu kuonesha kwamba hakutumwa kwa ajili yao. Ni wazi kwamba alitaka kumpima, kama mwalimu wakati mwingine aliwajaribu wafuasi wake, ila kwakweli alikuwa tayari kujibu ombi lake lakini alijaribu kuweka kikwazo kwa Imani yake. Bilashaka Yesu alitaka mwanamke atambue utume wa kweli wa Yesu na kwamba Yesu ninani. Pia alimtaka atambue upendeleo wa Waisraeli katika mpango wa Mungu, utambuzi ambao utamfanya akiri umuhimu wake wa kujitegemeza kwa Mungu wa kweli.
Yule mwanamke kwa kumuita Yesu Mwana wa Daudi, tayari ameshamkiri yeye kama Mfalme wa kweli wa taifa ambalo lilishinda juu ya taifa la mababu zake- mkuu zaidi ya wale waliotenda makubwa katika taifa lake. Na sasa anakataa kwakutokukubali kwamba utume wa Yesu ni kwaajili ya Waisraeli kwanza na kwamba yeye ni wa pili baada ya Waisraeli; lakini, anaamini kwamba Yesu atakuwa na nguvu zaidi kuliko hata ya ile wanayohitaji Waisraeli. Yesu anajibu kwasababu ya Imani hii jasiri. Yesu ana mkate wakutosha kwa wana wa Israeli, lakini maelezo yanayofuata yanatoa hakika kwamba yanabaki mengi kwaaajili ya wengine. Sisi tunao muamini Kristo tumekuwa taifa teule la Israeli Mpya. Mathayo alitaka kuwaambia watu wake kwamba, Waisraeli na wasio Waisraeli wote wanaweza kumfuata Mungu kwa Imani ndani ya Masiha, Kristo.
Sala:
Bwana, naomba watu wote wahisi upendo wako kwao kwa kupitia mimi.
Amina
Maoni
Ingia utoe maoni