Jumanne, Julai 31, 2018
Jumanne, Julai 31, 2018,
Juma la 17 la Mwaka wa Kanisa
Kumbukumbu ya Mta. Inyasi wa Antokia
Yer 14: 17-22;
Zab 78: 8-9, 11, 13;
Mt 13: 36-43.
KUKUWA KATIKATI YA MAGUGU
Injili ya leo inatualika kutafakari juu ya Ufalme wa Mungu. Yesu alikuja kutangaza na kuanzisha Ufalme wa Mungu. Somo la kwanza lina tukumbulisha ujumbe huu kwa kutangaza nguvu na mamlaka ya Mungu, ambaye ni mkarimu na mwenye huruma. Ingawaje ni mkuu juu ya yote anaongea na Musa uso kwa uso kama rafiki. Anatupa muda kuchagua kuwa katika ufalme wake.
Katika mfano wa magugu na ngano, yote yanakuwa pamoja, yote yanapokea Baraka kipindi cha uhai wao, lakini mwishoni wakati wa mavuno yanatenganishwa na kila moja litaonesha matunda yake. Wengi wetu tumebarikiwa kuzaliwa katika familia ya Kikristo. Mungu ametupatia Baraka ya ubatizo hata kabla hatujauelewa maana yake. Anaendelea kutupatia Baraka kwa njia ya kanisa. Lakini Baraka za kuwa mkristo haina maana tutaenda tuu mbinguni bila kujishughulisha. Uzuri ni kwamba Mungu ametupa uhuru wa kumchagua yeye au kumkataa, wakati wa mavuno itadhihirika kama ulimchagua Mungu au la! .
Tujaribu kufikiria kama Yesu alikuwa aje kesho na atawachukua wale wote wenye haki? Je, wewe utakuwa na wasiwasi? Pengine hapana. Au pengine kutakuwa na muda wa kutazama nyuma na kuwa na Amani na kuona haki inakuja. Mungu daima yupo katika kuongoza. Anatambua anafanya nini na atakuwa na utukufu juu ya vyote.
Wakristo wanaitwa waweze kuwa kama chachu katika jamii ili ulimwengu uweze kuwa sehemu nzuri ya kukaa. Kama sisi ni mashahidi wa kweli wa Kristo, Injili itaenea daima kila mahali. Kuingia kwetu katika ufalme itategemea kuchagua wema na kuacha yale yalio machukizo mbele ya Mungu. Wito wetu kama Wakristo tumeitwa kuwa mwanga wa ulimwengu, chumvi ya ulimwengu, ngano kati ya magugu, na ushuhuda wa upendo wa Yesu ulimwenguni. Tunaomba hii iwe sala yetu kwa Yesu kwani, ili mioyo mingi iweze kutambua uwezo upendo wa Mungu na kuwa raia wa Ufalme.
Sala:
Bwana Yesu, ninakuomba unisaidie mimi niweze kukaza macho yangu kwako na katika ushindi wa mwisho. Nisaidie mimi niweze kuwa mvumilivu nikwepe maovu ya ulimwengu huu kwa neema utakazo nipatia. Ninakuomba nisisahau ahadi yako siku ya mwisho uliioongea kwetu. Yesu nakuamini
wewe.
Amina
Maoni
Ingia utoe maoni