Ijumaa, Julai 27, 2018
Ijumaa, Julai, 27, 2018,
Juma la 16 la Mwaka wa Kanisa
Yer 3: 14-17;
Zab 83: 3-6, 8, 11;
Mt 13:18-23.
TULIOSIMIKWA KWA KRISTO
Injili ya leo inatualika leo tumtafakari Yesu kama mpanzi mwenye kusia Neno la Mungu. Yesu anatualika leo tusikilize neno la Mungu na tuongozwe na Neno hilo ili liweze kuzaa matunda. Mfano wa Mpanzi unaonesha nguvu ya neno la Mungu na nguvu kwa wale wanaolipokea na kulitii. Mfano wa Mpanzi unawahusu pia Wakristo wote walio na kazi ya kusia mbegu ya neno la Mungu kwa wengine wao kuwa kama vyombo vya Yesu.
Sisi kama wakristo tupo katika mfano na tunajulikana kama, mbegu zilizo anguka njiani, kwenye mwamba, kwenye miiba na kwenye udongo mzuri. Wakristo wasio ota katika udongo mzuri wanakosa mizizi. Wanatangaza Imani ya Yesu pale tu inapo pokelewa na wengine, na wakati ambapo mambo ni mazuri. Lakini mara wanapopata changamoto kwenye Injili, na kwenye neno la Mungu na hata pale kumfuata Kristo kunapo onekana hakupendwi. Mtu huyu huchagua kitu kingine na kukata tamaa. Hili ndilo linalojiri katika maisha yetu sasa. Tamaduni na ulimwengu vyote viwili vinakuwa vikali sana juu ya Injili ya Kristo na Imani Kikristo kwa ujumla. Ulimwengu unakuwa wenye nguvu, maarufu, na unaonekana kushinda vita. Udhaifu mkubwa ni kwamba wapo wakristo wengi wanaokosa mizizi ya Imani katika maisha yao ya Imani.
Ukweli ni kwamba tunapaswa neno la Mungu lisiwe ndani ya mioyo yetu palipo na udongo mzuri. Hili likifanyika neno litakuwa na kuzaa matunda. Na hata katika dhoruba ya ulimwengu na tamaduni zake Imani haitatikiswa. Tutafakari kama sisi tupo tayari kusimama na Kristo. Tuombe Mungu asie neno lake ndani ya mioyo yetu ili tusiyumbishwe hata kama tukipata dhoruba kali namna gani.
Sala:
Bwana, ninatamani kwamba neno lako lizame zaidi ndani ya moyo wangu. Ninatamani kusimama imara haijalishi ni dhoruba ya namna gani. Ninakuomba unisaidie mimi niweze kujitoa kwa ajili ya Imani yangu na katika mambo yote. Yesu nakuamini wewe.
Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni