Jumatano. 27 Novemba. 2024

Tafakari

Jumatano, Julai 18, 2018

Jumatano, Julai 18, 2018.
Juma la 15 la Mwaka

Isa. 10: 5 – 7, 13 – 16
Zab. 94: 5 – 10, 14 – 15 (K) 14
Mt 11:25-27

SIRI YA UFALME WA MUNGU ILIYO FUNULIWA KWA WATOTO!
Tunatambua sisi wote kwamba watoto wadogo wapo makini sana. Hasa wanapo kutana na watu wakarimu na wenye upendo, wana hisi mara moja na wanavutiwa kwao. Watoto wana waamini wakubwa. Kwahiyo kutoka katika hali hii ya watoto, uhusiano wetu na Mungu unapaswa kujikita katika hali hii na sio kumweka katika majaribu! Katika Injili Yesu anasema, vitu vyote amekabidhiwa na Baba yake. Ni kwasababu ana mwamini Baba yake bila kujibakiza.
Yesu anashuhudia kwamba Baba anawafunulia mambo yake wale walio kama watoto wachanga. Chakushangaza ni kwamba anasema, Baba amewaficha mambo haya wale wenye hekima na akili”. Lakini hii ina maana kwamba sio vizuri kujiona watu ambao tunafahamu kila kitu na kwamba tuna kila kitu. Sio vizuri kujazwa na majivuno na kujiona una majibu yote. Hatupaswi kusahau nini maana ya kuwa kama watoto wachanga. Haijalishi ni msomi namna ghani lakini twaweza kuwa wajinga sana. Hekima na akili haina thamani kama hatuna Imani kwa Mungu kama watoto wachanga wanavyo waamini wazazi wazuri. Haijalishi nina elimu namna ghani, hatuwezi kumpita Mungu. Mungu daima ni mwenye hekima, mwenye nguvu, na mwaminifu daima! Maisha hayapaswi kuchanganywa, yanapaswa kuwa ya kawaida.
Tafakari leo, ni kwa jinsi ghani ulivyo tayari kumrudia Mungu kwa moyo wa unyenyekevu hasa kwa maswali magumu katika maisha. Tafakari ni kwa jinsi ghani ulivyo tayari kumgeukia kwa Imani na matumaini ukifahamu kwamba Mungu daima ana majibu katika maisha yetu ya kila siku.

Sala:
Bwana, ninakuja tena kwako kwa kukuamini. Nisaidie mimi nitambue kuwa hekima yote inatoka kwako Baba na sio kwangu. Nisaidie mimi nikugeukie wewe daima kama mtoto na nisaidie maisha yangu yabaki ya kawaida kama unavyo tamani. Yesu, nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni