Jumatano. 27 Novemba. 2024

Tafakari

Ijumaa, Juni 22, 2018

Ijumaa, Juni, 22, 2018,
Juma la 11 la Mwaka

2 Fal 11: 1-4, 9-18, 20;
Zab 131: 11-14,17-18;
Mt 6: 19-23

MTUMAINI KRISTO KWANI ATAKUOKOA
Biblia ina ujumbe ndani yake ambazo kwa haraka haraka unaona hazipaswi kukaa katika Biblia Takatifu. Somo la kwanza ni moja wapo ya ujumbe hizo ambazo zinaongelewa kuhusu vita, umwagaji wa damu, shutuma, kukataliwa. Kwahiyo ni vizuri kuelewa nini uhusiano ujumbe huu. Vita kati ya falme na falme au shutuma na kukataliana ndani ya familia za kifalme yalikuwa mambo yaliojiri katika siasa za kipindi cha Agano la Kale. Biblia ni Historia ya moja wapo ya falme hizi-Israeli. Ingawaje, historia hii ilichukua umuhimu zaidi katika historia ya Waisraeli lakini matukio haya yanaelezewa katika mwanga wa mpango wa Mungu juu ya watu wake. Kwahiyo, kushinda au kuanguka kwa wana Waisraeli katika vita ni alama ya uaminifu wao au kutokuwa waaminifu kwa Mungu. Ushindi katika vita ni alama ya uaminifu kwa Mungu, na kushindwa katika vita ni kukosa uaminifu Kwa Mungu. Kwahiyo waandishi wa Biblia walipenda kuelezea ujumbe huu kwakutumia ishara hizo.
Je, ni ujumbe ghani tunapata kutoka somo hili la kwanza? Malkia Athalia kwakukosa uaminifu alichukua ufalme wa Yuda kwakuharibu familia zote za kifalme. Lakini hata hivyo Mungu alimlinda na kumuokoa mtoto mmoja wa kwanza wa Mfalme aliyeuwawa, ambaye alikuja kuwa alama ya matumaini. Ujumbe ni kwamba walio waovu hawataongoza siku zote, siku moja Mungu lazima atamleta mkombozi. Kwahiyo, mtumainie Mungu naye atakuokoa. Kwa upande mwingine, ujumbe huu pia unaeleza tena maana nyingine muhimu. Unatoa pia ujumbe na taswira ya baadae ambayo Mungu ataileta ya ukombozi kupitia mwanaye Yesu Kristo. Kama vile Mungu alivyowaokoa watu wake kutoka kwa kiongozi mbaya, vivyo hivyo Mungu atawaokoa watu wake kutoka katika utawala wa muovu-dhambi. Kwahiyo kwa kumuokoa mtoto Yoashi kutoka katika mikono ya Athalia, inatukumbusha kuhusu mtoto mwingine pia aliyeokolewa kutoka kwa mikono ya Herodi, ambaye alikuwa na kuongezeka katika hekima na kuwakomboa wanadamu wote-ambaye ni Yesu Kristo.

Sala:
Bwana, haijalishi nimeteseka namna ghani, au ni mateso ya namna ghani, naomba nisipoteze tumaini langu kwako juu ya neema yako Ee Bwana Mkombozi wangu.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni