Jumatano. 27 Novemba. 2024

Tafakari

Jumamosi, Juni 16, 2018

Jumamosi, Juni 16, 2018,
Juma la 10 la Mwaka

Kumbukumbu ya Mama Bikira Maria

1 Fal 19:19-21;
Zab 15: 1-2,5,7-10;
Mt 5: 33-37.


NDIYO

“Ndio yako iwe ndio na Sio yako iwe Sio. Zaidi ya hapo yanatoka kwa muovu” (Mt 5:37). Huu ndio mstari unaogusa sana. Zaidi sana inaonekana kuwa baada ya kusema kinachotoka zaidi ya hayo kinatoka kwa yule muovu”. Lakini kwasababu haya ndiyo maneno ya Yesu yapo katika hali ya ukweli mtupu. Yesu ana maana gani?

Maneno haya ya Yesu yanakuja kwetu katika hali ya kufundisha kuhusu hali ya kuchukua kiapo. Somo hili maana yake limejikita katika hali ya “ukweli” unaopatikana katika amri ya nane. Yesu anatuambia sisi tuwe waaminifu, katika kusema na tuna maana gani na kumaanisha tunachosema.

Sababu moja wapo kwanini Yesu ameleta hili., katika hali yake yakuongelea kuhusu kiapo, Yesu ana maana kwamba, haina haja ya kiapo katika mazungumzo yetu ya kila siku. Katika kila sakramenti kuna aina ya kiapo inayochukuliwa. Lakini katika kiapo hiki ni aina ya kuonesha Imani.

Ukweli ni kwamba amri ya nane ambayo inatuhitaji sisi tuwe waaminifu na watu wa kweli inapaswa kutawala katika maisha yetu ya kila siku. Hatuhitaji “kuapa kwa Mungu” kuhusu hili au lile. Hatuhitaji kuapa au kuhitaji kujitetea kuwaeleza wengine kwamba tunasema ukweli katika hali hii au ile. Bali, kama sisi ni watu wa ukweli na uaminifu, maneno yetu yatatawala na kila tunachosema kitakuwa kweli kwasababu tunamaana hiyo.

Tafakari, leo wewe ni mwaminifu kiasi gani katika Nyanja zote za maisha. Je, umejenga hali ya ukweli katika Nyanja zote za maisha? Je, watu wanatambua hadhi hii katika maisha yako? Kuongea ukweli na kuwa mtu wa ukweli kutangaza ukweli wa Injili katika matendo yetu. Jikite katika ukweli leo na Bwana atafanya mambo makubwa katika maneno yako.

Sala:
Bwana, nisaidie mimi niweze kuwa mtu wa kweli na mwaminifu. Saidia “ndiyo” yangu ili iweze kuwa kadiri ya mapenzi yako matakatifu na nisaidie daima niondokane na njia za upotovu.
Amina .

Maoni


Ingia utoe maoni