Jumatano. 27 Novemba. 2024

Tafakari

Jumatano, Juni 13, 2018

Jumatano, Juni, 13, 2018,
Juma la 10 la Mwaka wa Kanisa

Kumbukumbu ya Mt. Antoni wa Padua,( Padre na Mwalimu wa Kanisa)

1Fal 18:20-39;
Zab16: 1-2, 4-5, 8, 11;
Mt 5:17-19.


SHERIA YA UPENDO!
Katika Injili ya leo, Yesu kwa hakika anawahakikishia wanaomsikiliza kwamba, “hakuja kutengua sheria na manabii. Nimekuja si kutengua bali kuikamilisha”. Yesu alikuja si kuifuta sheria bali aiinue katika hali ya juu ya ukamilifu. Mtazamo wa Yesu unatusaidia tuione sheria katika mwanga mpya. Maneno yake ni kwa ajili ya kufariji lakini pia yanaleta changamoto, akionesha njia inayoenda juu sana kuliko sheria mpaka kwenye sheria ya Upendo. Sheria isiyo na upendo haiwezi kulinda utu na maisha ya mwanadamu. Inamfanya mwanadamu awe kama aina fulani ya kitu kisicho na uhai. Yesu anatutaka tuwe na upendo zaidi. Pengine wakati mwingine tunasisitiza mno sheria kiasi cha kushindwa kuonesha upendo na msamaha kwa wengine.

Katika maisha yetu, tunapaswa kuwa tayari kusonga mbele tukiwa wabunifu wa njia mpya za kuweza kutufanya tuelewe na kuishi Imani yetu zaidi. Tamaduni zetu na mapokeo yetu ni mazuri na tusiyapoteze lakini pia tutumie hali hiyo hiyo katika kuelewa na kuangalia hitaji la sasa.

Sala:
Bwana Yesu, ifanye imani yetu iwe mpya kila siku katika mwanga wa sheria zetu na mapokeo yetu na katika njia ya sheria ya Upendo.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni