Jumatano. 27 Novemba. 2024

Tafakari

Jumatatu, Juni 11, 2018

Jumatatu, Juni 11, 2018,
Juma la 10 la Mwaka

Kumbukumbu ya Mt. Barnaba Mtume.


Mdo 11: 21-26, 13: 1-3;
Zab 97: 1-6;
Mt 10: 7-13

PEANENI MOYO!

Barnaba alikuwa mtu muhimu katika kanisa la mwanzo, ingawaje sio mmoja wa wale mitume kumi na mbili aliyokuwa nao Yesu katika karamu ya mwisho, yeye alipata cheo cha mtume. Uwepo wake unaonekana kuwa muhimu katika sura kumi na tano za mwanzo za kitabu cha Matendo ya mitume. Aliuza mali zake zote na akaleta yote kwa mitume (Mdo 4: 37). Alikuwa akijulikana kama Yosefu kutoka Cyprus, lakini mitume walimpa jina la Barnaba ( maana yake mwana wa kutia moyo), ukweli uliopo katika jina hii, aliwatia moyo watu wa Yerusalemu wa mpokee Saulo kwasababu sio tena mtesi wa kanisa baada ya kuongoka (Mdo 9: 27). Wakati idadi kumbwa ya Wasamaria ilipo ongoka nakupokea Ukristo katika Antokia ya Siria, Jumuiya ya Yerusalemu walimtuma kwenda Antokia kuhakikisha na kuangalia hali halisi. Barnaba aliijua neema ya Mungu alipoona na kuwatia moyo jumuiya hii mpya kwa maendeleo mazuri (Mdo 11: 19-26).

Jumuiya ya Antokia waliwachagua Paulo na Barnaba kuwa watu wakwanza kwa safari ya kimisionari, kutoka kati ya “manabii na walimu” ili wafanye kazi ya Roho Mtakatifu (Mdo 13 na 14). Katika utume Barnaba alifuatana na Paulo mtu wa haki. Ingawaje baadae kulikuwa na mgongano kati yao. Waligawa jumuiya walizo zianzisha. Katika hili tunaona ubinadamu kama sisi katika nguvu na madhaifu. Tukijikita wenyewe katika kazi ya Mungu, Roho Mtakatifu atatutumia mpaka mwisho wa kilele cha nguvu zetu, licha ya madhaifu yetu.

Mt. Barnaba anatufundisha kitu katika maisha yetu kama wafuasi wa Kristo, tuwe na moyo wa kushirikisha yale aliyotujalia Mungu pasipo choyo. Tuwe tayari kuwatazama jirani zetu kwa yale aliotujalia Mungu. Barnaba aliuza yote aliokuwa nayo akaleta kwa Mitume ili jumuiya yote ya waumini iweze kufaidika kwa majitoleo yake. Katika jumuiya zetu ndogo ndogo wakati mwingine tunasali pamoja, tunacheka pamoja baada ya sala na kupanga mipango mbali mbali. Pengine tujiulize katika mipango yetu tunapata muda wa kuwajali maskini na wasio jiweza walio kati yetu? Na pengine tumesali nao? Au tunafurahi kucheka nao bila kujali wanaishi je? Na pengine mnapotofautiana katika mawazo mnatafuta njia sahihi ya kurudisha tena upendo kati yenu? Au mnaishi kwakununiana ili mradi nimekuja tuu jumuiya nimeonekana ili na wao waje kwangu kipindi kingine? Ndugu zangu, mipango yetu katika jumuiya zetu isimtenge mtu au kumuona mmoja kati yetu ni bora zaidi ya mwingine. Tufanye yote kwa umoja tukiwajali wale wasio nacho kama jumuiya ya kwanza ya Yerusalemu. Tuwe kama Barnaba tuwafariji wengine na kuona uzuri pia ndani ya wengine, tuwape moyo ili wasikate tamaa. Mungu amatupa vipaji tofauti tuviunganishe vyote kwa pamoja ili vikamilishane vijenge jumuiya yenye nguvu, mmoja asijione kuwa yeye ndio kila kitu. Tushirikiane kwa upendo tukichukuliana kwa furaha na Amani ili ufalme wa Mungu uwe kati yetu.

Sala:
Nisaidie mimi Bwana, niwatie moyo na kushirikiana na wenzangu katika kujenga kanisa lako.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni