Jumatano. 27 Novemba. 2024

Tafakari

Jumamosi, Juni 09, 2018

Jumamosi, Juni, 9, 2018,
Juma la 9 la mwaka wa kanisa

Kumbukumbu ya Moyo safi wa Bikira Maria

Is 61: 9-11 au 2 Tim 4: 1-8;
1 Sam 2: 1, 4-5 au Zab 71: 8-9, 14-17, 22;
Lk 2: 41-51 or Mk 12: 38-44.


MOYO UNAOMTAFAKARI MUNGU!
Leo tunasoma kwamba Yosefu aliichukua familia yake Yerusalemu kila mara wakati wa Pasaka, ili kutimiza sheria (wajibu wake). Yosefu na Maria walifanya safari ya siku tatu kutoka Nazareti kila mwaka. Ni kati ya safari hizi mtoto Yesu alipotea.

Katika injili ya leo tunaambiwa kuwa wazazi wa Yesu walimkuta Yesu hekaluni. Kukaa na kuongea ilikuwa ni kawaida kwa walimu wa sheria. Maswali na majibu ilikuwa ni aina ya utamaduni wa kufundisha kwa Wayahudi na Walimu wakiyahudi walishangazwa na hekima
ya maswali na majibu yaliotoka kwa mtoto wa miaka kumi na mbili. “Wote waliomsikia walishangazwa”. Mt. Luka katika Injili anataka kutuambia kwamba Yesu alikuwa ameshajiandaa tayari kwa kazi yake kama mwalimu hata katika umri wa utoto wake, mwenye hekima na mamlaka. Hatimaye tunaambiwa kwamba “Aliondoka nao wakarudi nazareti na alikuwa akiwatii”. Ingawaje alikuwa na asili ya Mungu “alishuka chini” kutoka katika hali hiyo ya juu ya roho na akawa kama mwanadamu. Somo kubwa sana kwetu! Maria aliyaweka haya yote ndani ya moyo wake na anatualika sisi tufanye hivyo. Je, tunampenda Maria awe nyota yetu yakukukutana na Mungu?.

Sala:
Bwana nisaidie mimi nikutafute wewe daima katika matukio yote ya kila siku katika maisha yangu na kuyaweka mafumbo haya moyoni mwangu kama Bikira Maria alivyofanya.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni