Jumatatu, Mei 28, 2018
Jumatatu, Mei, 28, 2018,
Juma la 8 la Mwaka .
1Pet 1: 3-9;
Zab 110: 1-2, 5-6, 9-10;
Mk 10: 17-27
KUWA TAYARI KUMFUATA YESU!
Katika Injili, tunasikia kuhusu habari ya tajiri mmoja, aliyeamini kwamba furaha yake ipo katika mali. Tunaweza tukajiuliza, kwanini ni vigumu kwa tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu? Je, kuna ubaya kuwa tajiri? Jibu letu linategemea maana ghani tuliyonayo kuhusu “Tajiri” na “Ufalme wa Mungu”. Wakati Yesu anapotumia neno “Tajiri” ana maana ya mtu aliye na vingi, vingi sana kuliko wale wanaomzunguka, na hasa zaidi wakati hao waliomzunguka hawana hata mahitaji muhimu. Watu kama hawa wanaoweka furaha yao kwenye mali zao na kufurahia kwa ubinafsi maisha ya juu wakati hao wanaomzunguka hawana chakula au nyumba, hili linakuwa haliendani na Yesu na Ufalme wake.
Pia, kuwa mfuasi wa Yesu, maana yake ananiuliza mimi nimfuate bila kuweka vipingamizi, bila kuweka vikwazo, kuwa tayari kuacha chochote na vyote. Hii ndio maana ya KUWA TAYARI. Tajiri katika Injili hakuwa ‘tayari’ kumfuata Yesu. Upo tayari?
Sala:
Bwana, naomba niishi maisha yangu, nikishirikisha yote niliyonayo na wale wasionacho. Naomba niwe tayari daima kukufuata.
Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni