Jumatano. 27 Novemba. 2024

Tafakari

Jumanne, Mei 22, 2018

Jumanne, Mei, 22, 2018,
Juma la 7 la Mwaka wa Kanisa

Yak 4: 1-10;
Zab 55: 7-11, 23;
Mk 9: 30-37.


KULENGA KILICHO CHA MUHIMU!

Leo tunawaona Mitume wakibishana juu ya nani aliyemkubwa kati yao. Hili pia ni jambo ambalo tunaliona pia katika familia zetu, jumuiya na jamii zetu. Je, sisi hatujiulizi/hatukujiuliza, hivi kati yetu mama anampenda nani zaidi? Au Baba anampenda nani zaidi? Ni kitu ambacho ni sehemu yetu kama wanadamu. Lakini leo Yesu akimtumia mtoto mdogo anawaambia, “mmoja wenu anayewakaribisha mmoja wapo wa watoto wadogo kama hawa kwa jina langu, anikaribisha mimi, na anayenikaribisha mimi, hanikaribishi mimi pekee bali amkaribisha yule aliyenituma mimi”

Yesu alikuwa akiongelea kitu ambacho kilikuwa kinampa uchungu mkubwa, mateso yake, kifo na ufufuko wake. Lakini cha ajabu mitume walikuwa wakishughulika na mambo yao binafsi. Watoto pia wao wanaweka muolekeo katika mambo madogo, huwa hawafikirii kujenga “maghorofa angani” kama wakubwa wanavyofanya. Wanaota, lakini wakati wanacheza, wanacheza. Wakati wanatazama TV mawazo yao na muelekeo wao wote upo kwenye TV. Katika ulimwengu uliojaa vitu vingi vya kutazama vinavyoharibu wakati mwingine kama vile simu, Tv, Internet, Yesu anatupa changamoto na kutuuliza, ni mara ngapi tumeweka muelekeo wetu kwake? Tupo makini kiasi ghani kuhusu mpango wa Mungu katika maisha yetu? Je, mipango yetu yote inalenga katika kupata maisha mazuri na kuishi vizuri hapa duniani tu? Au tunashughulika na maisha yetu na Mungu mbinguni pia? Je maisha yetu yanatuelekea sisi wenyewe tu au na Mungu pia?

Sala:
Bwana, naomba nielekeze maisha yangu katika lengo lako juu ya maisha yangu.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni