Jumatano. 27 Novemba. 2024

Tafakari

Ijumaa, Mei 18, 2018

Ijumaa, Mei 18, 2018,
Juma la 7 la Pasaka

Mdo 25: 13-21;
Zab 103: 1-2, 11-12, 19-20 (K. 19);
Yn 21: 15-19.

JE, WANIPENDA?
Katika lugha ya Kigiriki, kuna maneno tofauti yanayo tafsiriwa kama “Upendo”. Agape ni aina ya upendo uliyo kamilika, safi, usio na ubinafsi, upo hai. Agape maana yake, kujali na kuwapenda wote, na kujali bila kuweka nafsi mbele. Kuna upendo pia ambao ni hafifu (Phileo), kumpenda mtu kwasababu yakutaka kupendwa naye au kwasababu yakutaka kupata vitu au kitu fulani kutoka kwake.

Yesu anamuuliza Petro kwa mara zote mbili za kwanza, “je, Simoni wa Yohane, wewe wanipenda (Agape) kuliko hawa?” anasema “ndiyo Bwana, wajua nakupenda (Phileo).” Ingewezekanaje Petro aseme moja kwa moja bila wasi wasi Bwana nakupenda (Agape) baada ya kushindwa kwake kumkiri Bwana? Yesu anamuuliza mara ya tatu, Simoni mwana wa Yohane, je wanipenda (Phileo) mimi?” (angalia hapo Yesu amebadili upendo hapo kutoka Agape na kwenda Phileo). Petro “anahuzunika” si kwasababu tu Bwana alimuuliza mara ya tatu, bali ameshusha kiwango cha upendo, kutaka kumuonesha Petro upendo wake upo wapi!. Tunaweza kufikiri ni jinsi gani Petro alivyo huzunika moyoni. Isingekuwa ni kwasababu ya woga na hofu iliomkumba Petro wakati wa mateso ya Yesu, pengine kabla angeweza kusema kwanguvu zote kabisa, Bwana unaniuliza swali ghani? Bila shaka nakupenda (Agape). Lakini matendo yake yalionesha wazi ni kwa jinsi ghani alishindwa agape kwa Bwana. Alikana hata urafiki (phileo) na Bwana. Na sasa ana “huzuni” ya kweli wanavyo onana uso kwa uso na Bwana kwa yale aliyotenda.


Hili lina maana ghani kati yangu na wewe? Ina maana kwamba hatujachelewa sana. Tunaweza kuwa tumemkosea Bwana kabla, lakini kwa huzuni ya kweli, tuna nafasi nyingine yakumdhihirishia Yesu na sisi wenyewe, kwamba sisi ni Wakristo wa namna ghani. Tumejikuta tukimkana Yesu kwa kugeukia dhambi, turudi sasa na kumpenda kikamilifu (Agape).

Yesu anamuambia Petro pia alipokuwa kijana alipenda kwenda popote pale alipopenda, pengine hata sisi tujaribu kujiuliza, sisi tukiwa bado tuna nguvu zetu tunafanya nini? Tunatumia nguvu zetu kusali au tunasubiri mpaka tuwe wazee ndio tuanze kusali? Pengine unaweza kujipa kisingizio cha kazi, je unasubiri mpaka ustaafu ndio uanze kwenda kanisani? Tujiwekee hazina tukiwa bado tuna nguvu, ili uzee wetu uwe na Baraka. Tujipatanishe na Mungu daima tukiwa bado na nguvu zetu, tusimuache Mungu kamwe.

Sala:
Bwana, unafahamu kwamba nakupenda. Nafahamu unafahamu ni kwa jinsi ghani nilivyo dhaifu. Ninaomba nisikilize wito wa mwaliko wako wa kuonesha mapendo yangu kwako na hamu ya kupata huruma yako. Ninaomba nitoe upendo huu na hamu hii ya kupata huruma katika hali ya juu kabisa. Yesu, nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni