Jumatano. 27 Novemba. 2024

Tafakari

Jumanne, Mei 15, 2018

Jumanne, Mei 15, 2018,
Juma la 7 la Pasaka


Mdo 20: 17-27;
Zab 68: 10-11, 20-21(K. 33);
Yn 17: 1-11.


UTUME WA KUTIMIZA!
Paulo anauacha moyo wake uweze kuzungumza na wakubwa wa Kanisa. Kanisa lilikuwa katika hali ya uchanga, na lilihitaji watu watakao jitolea kweli kwaajili ya kulihudumia. Yesu mwenyewe alimchagua Paulo kuwa mmoja wa wahudumu wa kanisa. Kwakweli, Paulo, hakuishi uongo, hakuwa mtu wakutafuta faida binafsi. Alikuwa muhubiri wa kweli na muwazi, ambaye aliongea vizuri ujumbe wake ili aeleweke hata na wale wadogo kabisa. Alikuwa mhubiri maarufu, alihubiri Injili, alihubiri injili kama ushuhuda kwao wakipokea, na kama ushahidi juu yao kama watakataa. Alikuwa mhubiri aliyejiamini, aliyekuwa na lengo sio la kujulisha akili zao bali mioyo yao na maisha yao. Alikuwa mhubiri aliyefanya kazi kweli, mwenye utajiri mwingi kwa maneno yake, hakuchoka wala kuboreka. Alikuwa mhubiri mwaminifu. Hakuacha kukemea pale mambo yalipoenda tofauti, na kwa ujasiri akatangaza fumbo la msalaba.

Alikuwa mkristo wa kweli, hakuhubiri misemo yenye mashaka wala kufundisha falsafa ya juu yenye kupotosha, wala hakuingilia mambo ya nchi, au njia za kuongoza, lakini alihubiri Imani na toba kama alivyofanya mwalimu wake ambaye ni Yesu. Paulo alichukulia wito wake kama utume aliopewa na Bwana wake Yesu Kristo. Kwanjia hii aliuchukulia kuwa ni mtakatifu na wamamlaka kutoka juu. Kama Paulo sisi nasi tuna bado mbio za kukimbia, kazi ya kufanya. Tuna kazi maalumu tuliopangiwa. Tupo katika hali mbaya kama tutakataa na kuacha kazi yetu.

“Saa” anao ongelea Yesu ni muda wa kusulubiwa kwake ambao waweza kuonekana kama muda wa huzuni. Lakini katika hali ya Kimungu ni muda wa utukufu. Ni muda wa kutukuzwa na Baba yake wa Mbinguni kwasababu alitimiza mapenzi ya Baba yake katika ukamilifu wote. Alipokea kifo chake kwa ajili ya wokovu wa Ulimwengu. Wasaa wa Yesu ni muda ambao tunapaswa kuuishi kila wakati, kwa kubeba misalaba yetu ya kila siku. Kwa kufanya hivyo misalaba yetu inatakatifuzwa kwa nguvu za Kimungu na kuwa sehemu ya kupata neema za Mungu. Uzuri wa Injili ni kwamba kila msalaba tunao vumilia au kubeba, ni muda wa kudhihirisha msalaba wa Yesu. Tunaitwa na yeye kwa kumpa utukufu kwa kuishi mateso yetu na kifo chetu siku zote za maisha yetu. Kufa katika dhambi na kufufuka katika neema.

Sala:
Bwana Yesu, tupe nguvu tuweze kuvumilia katika magumu yetu yote ya maisha. Tunaomba yote yawe sehemu ya kukupa utukufu. Tunaomba tuwe kama Mt. Paulo, kwa kuwa waaminifu katika utume uliotupatia sisi. Yesu, nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni