Jumapili, Aprili 29, 2018
Aprili 29, 2018.
------------------------------------------------
JUMAPILI, DOMINIKA YA 5 YA PASAKA,
Somo la 1: Mdo 9: 26-31 Barnabas anamtambulisha Paulo ambaye ameongoka kwa waamini wa Yerusalemu. Walimpokea lakini Wayahudi walijaribu kumuua.
Wimbo wa Katikati: Zab 22: 26-28, 30-32 Moyo wangu utaishi nae na watoto wangu watamtumikia yeye.
Somo 2: 1 Yn 3: 18-24 Kama tunataka kuishi kama Mungu anavyopenda, tunapaswa kushika amri zake, hasa amri ya kuwapenda wenzetu..
Injili: Yn 15: 1-8 Akitumia ishara ya Mzabibu na matawi, Yesu anaelezea umoja wake wa ndani pamoja nasi.
------------------------------------------------
KUUNGANIKA NA YESU
Mmisionari alikuja Afrika ya akawa anaishi sehemu moja ambayo umeme ulikuwa hautoshi kusambazaa kanisani kwake na maeneo mengine. Baadhi ya watu wa eneo lile walienda kumtembelea huyu Padre. Walitambua kuna balbu ilikuwa imeninginia kutoka chumba chake alichokuwa akiishi. Wakawa wanamwangalia jinsi anavyoweka hiyo taa na jinsi anavyowasha na kuwaka. Mmoja wa wale waliokuja kumtembelea akamuomba kama na yeye anaweza kuwa na babu ya namna hiyo. Huku Padre akidhani kwamba pengine anataka tu kwa ajili ya kuchezea au kuangalia aliamua kumpatia balbu ambayo imeungua. Siku moja Padre alivyokuwa akienda kwenye utume wake akasimama katika nyumba ya yule aliemuomba balbu. Yule Padre akashangaa akaiona ile balbu ikiwa inanginia katika nyumba ya huyu mtu! Na hapo alibidi aanze kuelezea kwamba ili ile balbu iwake inabidi wawe na nguvu ya umeme na waya wakuleta umeme kwenye ile balbu. Bila kuunganisha huwezi kupata mwanga!
Siku ya Alhamisi kuu Yesu alikula chakula cha pekee na wafuasi wake-chakula cha Pasaka. Kilikuwa ni chakula cha mwisho kabla hajaingia katika mateso na kufa. Kifo kilikuwa kinanyemelea. Kulikuwa ni hatari kila upande. Ilikuwa ni ngumu kutambua ni yupi wa kumwamini. Yeye mwenyewe alilihisi hili zaidi kuliko hata wao wenyewe. Wakati huu Yesu alihisi kuwa karibu na mitunme wake kuliko muda mwingine. Kutaka ni kwa jinsi gani alivyokuwa anahisi aliamua kushuka chini na kuwaosha miguu. Na hapo aliongea nao kwa uchungu kutoka moyoni kwamba ni kwa jinsi gani mmoja atamsaliti, na kwa jinsi gani wengine watatawanyika.
Umoja aliouhisi Yesu usiku ule na wafuasi wake umeendelea kuwapo daima. Akiwa njia katika bustani ya Gestemane, alipata uchungu wa umoja wake pamoja nao. Alisimama karibu na mzabibu na kuwaambia “mnaona mzabibu huu, angalieni umoja uliopo kati ya shina na matawi yake, ndivyo ilivyo kati yangu na ninyi. Mimi ni mzabibu nanyi ni matawi. Kama utabaki ukiwa umeungana nami utazaa matunda mengi. Lakini kama hamtabaki mkiwa mmeungana nami hakika mtakauka.” Hivi ndivyo Yesu alivyohisi. Hivi ndivyo Yesu alivyopenda kati yake na wafuasi wake. Ndivyo anavypenda na sisi tubaki tukiwa tumeungana naye. Yeye ni mzabibu nasi ni matawi. Hatupaswi kusubiri wakati wa hatari na matatizo alafu tunaacha kuungana na huu mzabibu. Tunapaswa kuwa ni sehemu yetu ya kushi daima.
Yesu alipenda wafuasi wake watambue hilo ili watengeneze Jumuia yenye mapendo. “Mimi ni mzabibu na Baba yangu ni mkulima yeye huondoa kila tawi lisilo zaa matunda. Kila tawi linalozaa matunda Baba yangu hulichenga vizuri ili lipate kuzaa matunda mengi ajabu”. Kwanza kabisa sisi tunakumbushwa kwamba Baba ndiye mkulima. Yeye ni chanzo cha Uzima wa Yesu na Kanisa lake na kwa jinsi hiyo sisi tumeunganika na Yesu na hivyo tunakuwa na kuzaa matunda. Haitakiwi kuwe na tawi linalojitafutia mambo yake. Tawi hilo likiwa hivyo litasinyaa na hivyo litakatwa.
Kupruni wakati mwingine kunauma, katika kanisa inaweza kuwa ni kuacha baadhi ya shughuli zako na kufanya mambo yakuendeleza kanisa, ili kanisa zima liweze kusimama(mzabibu). Ukuwaji mwingine unaweza kuzuia mzabibu ushindwe kuzaa matunda. Sisi wote tunahitaji, kupruniwa, kusahihishwa, kuongozwa, kuwa na heshima ili maisha yetu yaweze kuzaa matunda. Kupruni huku ni muhimu sana hasa kwa wale watu ambao wameshafanikiwa katika maisha yao ya Kikristo ili wasirudi nyuma waendelee kuzaa matunda mengi. Njia pekee ya kuzaa matunda ni kuhakikisha sisi tumebaki tukiwa tumeunganika na Yesu. Na kutambua sisi tunamtegemea Mungu kwa kila kitu, hata maisha yetu yote. Kipindi cha Pasaka ni sikukuu ya kusherekea kuungana na Yesu. Waamini wengi tumekuwa wasaanii wa Imani na hivyo tunaweza kuishia kutafsiri Injili katika muonekano wa nje tuu. Leo tunahimizwa kuhakikisha tumejiunga na Yesu kweli kweli.
Katika somo la kwanza Paulo anafanya kazi ya Mungu na sasa Yesu ameamua kumuunganisha naye ili asije akawa tawi lisilo zaa matunda. Barnaba anamtambulisha kwa waumini wa Yerusalemu waweze kumpokea kama moja la tawi katika shina la Kristo. Nasi tuwatafute wenzetu ambao hawapo katika shina ili waweze kujiunga na sisi kwa pamoja tuweze kuwa watoto wa Mungu kama Yohane anavyotuambia katika somo la Pili . kwamba tukiwa na upendo kati yetu basi sisi tutadhihirisha kwamba sisi ni watoto tulioshikamana katika shina moja la Yesu na hivyo sisi wote tunakuwa wana wa Mungu.
Sala:
Bwana kama vile matawi yanavyo jiunga na shina, ninakuomba mimi nijiunge newe Ee Bwana.
Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni