Alhamisi. 21 Novemba. 2024

Tafakari

Jumatano, Septemba 07, 2016


Jumatano, Septemba 7, 2016.
Juma la 23 la Mwaka


1 Kor 7: 25-31;
Ps 44: 11-12, 14-17;
Lk 6: 20-26


KIU YA KUTAKA FURAHA!

Kila moyo wa mwanadamu umeumbwa kwa ajili ya furaha. Mungu mwenyewe, katika Utatu Mtakatifu, ndiye Furaha Kuu, ndiye Furaha yote. Masomo yetu ya leo yanatuambia kwamba maskini wapo katika hali salama zaidi kuliko matajiri. Moyo wa Mwanadamu, na uzuri wake na uwezo wake wakupata utakatifu, unachafuliwa, unazimwa na kuharibiwa kwa kuwa mtumwa wa mali na anasa. Tamaa isiyo na mpangilio ya fedha, nyumba, ardhi na vitu vimechafua furaha ya watu wengi na pia furaha ya familia mbali mbali.

Leo Injili inaongelea pia kitu kingine kinachochafua roho nyingi: tamaa ya anasa na kusifiwa (kijenga jina). “Ole wenu ninyi watu wote watakapo wasifu, kwakuwa baba zao waliwatenda manabii wa uongo mambo kama hayo” (Lk 6: 26). “heri yenu ninyi watu watakapo wachukia, na kuwatenga, na kuwashutumu, na kulitupa nje jina lenu kama neno ovu, kwa ajili ya Mwana wa Adamu. Furahini na kuruka-ruka, kwakuwa, tazama, thawabu yenu ni kubwa mbinguni, maana, baba zao waliwatenda manabii [WA KWELI] vivyo hivyo.” (Lk 6: 22-23).

Yesu anataka kutuambia kwamba watu wakweli wanaomfuata watapata mateso mengi, haitakuwa rahisi njia ya Yesu, mtu anapaswa kusema ukweli hata pale inapo hatarisha maisha yake, kama vile manabii wa ukweli walivyoteseka zamani. Sifa za nabii wa ukweli ni kwamba hakuambii kile ambacho unachotaka kusikia bali anasema ukweli kwasababu ni ukweli. Manabii wengi walipoteza maisha yao kwasababu waliitwa na wafalme ili kutoa unabii juu ya jambo Fulani, lakini wao kwa ujasiri walisema ukweli hata kumrekebisha mfalme na hapo maisha yao yakawa hatarini. Mfalme alitegemea kusikia akisifiwa tu, lakini manabii wa kweli walisema ukweli, huu ndio wito anaotuambia Yesu. Tusiwe kama nmanabii wa uongo wanaopenda kuongea tu kile ambacho watu wanapenda kusikia bali tuseme ukweli kwasababu ni jambo la kweli.

Sala: “Umetuumba kwa ajili yako mwenyewe, ee Bwana! Na roho zetu hazitatulia mpaka zitakapo tulia kwako.” (Mt. Agustino) Amina

Maoni


Ingia utoe maoni