Jumatano. 27 Novemba. 2024

Tafakari

Jumatatu, Aprili 02, 2018

Jumatatu, Aprili 2, 2018.
Oktava ya Pasaka

Mdo 2:14,22-32
Zab 16:1-2,5-11
Mt 28:8-15.


KUMWABUDU BWANA MFUFUKA!

Habari kuhusu Yesu mfufuka zinaleta hali mbili kwa wale wanaosikia kuhusu habari hii hapo kwanza. Moja ni muelekeo wa kumfuata Yesu mfufuka na nyingine ni muelekeo wa kukataa kuhusu Yesu mfufuka. Wakati wakina Maria na wenzao walikuwa na furaha ya kutangaza habari hii njema ya ufufuko, viongozi wa Wawayahudi wanahofu na wanaogopa kuhusu kukiri na kukubali habari hizi. Wakati wakina Maria wanatafuta kila njia na namna ya kumweleza kila mtu kuhusu habari hii njema ya ufufuko wa Bwana, Viongozi wa Wayahudi wanatafuta njia ya kuificha habari hii njema isienee kwa kwa watu.

Leo ni siku ya pili katika oktava ya Pasaka. Ina maana kwamba leo ni Pasaka. Tunasherekea siku ya Pasaka kwa mfululizo wa siku nane na kuingia katika jumapili ya Huruma ya Mungu. Hivyo siku hizi nane ni siku ambazo tunapaswa kubaki na kutafakari kwa undani kabisa na kuhisi kama hawa wanawake watakatifu baada ya kutambua kwamba Yesu hayupo tena kaburini amefufuka. Tunapaswa kujiachia wenyewe tuingie kwenye mafumbo ya ufufuko. Tunapaswa kuyaona kama yalivyo. Tunapaswa tutazame zawadi hii, na mshangao wa hakika wa ufufuko, Yesu ameangamiza matokeo ya dhambi. Aliangamiza kifo chenyewe.

Wakati hawa wanawake wakitoka kaburini, maandiko yanatuambia kwamba walikutana na Yesu mfufuka wakiwa njiani. Na yanasema kwamba walimuona Yesu, na walimkaribia na kuishika miguu yake, na kumwabudu”. Hili sio tendo dogo la kuabudu na upendo. Kitendo hichi cha kumtukuza na kumwabudu Yesu kinaonesha kwamba hawaku muamini tu, bali walimwabudu. Tunapaswa kufanya hivyo, kama wao.

Tutumie muda huu wa Oktava ya Pasaka na kutafakari juu ya ufufuko na kuwa na muda juu ya unyenyekevu wa kumwabudu Yesu. Tujiachie wenyewe tuje mbele ya Yesu uso kwa uso, na kumwacha yeye mwenyewe abadilishe maisha yako.

Sala:
Bwana, nina amini. Nina amini kwamba umefufuka kwa ushindi juu ya dhambi. Ninakuomba unisadie kuelewa na kuhisi hali hii ya utukufu wa ajabu katika maisha yangu. Ninakuabudu kwa upendo usio pimika, Bwana mpendwa. Nisaidie nikuabudu wewe kwa hali yangu yote. Yesu, nakuamini wewe.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni