Jumatano. 27 Novemba. 2024

Tafakari

Ijumaa, Machi 30, 2018

Ijumaa, Machi 30, 2018,
Juma Kuu
IJUMAA KUU

Isa 52:13-53;
Zab 31:2,6,12-13,15-17,25
Ebr 4:14-16, 5:7-9;
Yn 18:1 - 19:42


MTAZAMENI MTU!
Ni Ijumaa kuu, siku ambayo ilikuwa muhimu sana kwa Yesu kwa lengo lake la kuja ulimwenguni. Maisha yake yote, mafundisho yake yote, kila neno la msamaha au changamoto hakuna lolote linalo leta maana kama bila msalaba. Na leo tunaitwa kujiunga na mamilioni ya watu duniani kote kwa kumtazama Mwanakondoo wa Mungu aliye sulubiwa kwa ajili ya dhambi zetu.

Kwa maneno ya Pilato. “Mtazameni mtu”, tumtazame Kristo, tukitazama na kurudi katika unyenyekevu wake wa kuzaliwa katika zizi. Tukikumbuka miaka yake aliokuwa akikuwa katika hekima na kimo. Tumuone katika unyenyekevu wake, muamini na kujikabidhi kwa Baba yake, alivyotembea na Mungu katika kila hatua ya maisha yake. Tazama aliyesali mikononi mwako naiweka roho yangu. Tazama sala hii aliyoisema wakati akivuta pumzi yake ya mwisho ilivyokuwa, lakini maisha yake yote yaliojikita ndani ya Baba yake.

Njooni na “tazama aliyesema naona kiu”, tazama aliye ona njaa, kiu, ndani ya mwili na roho. Hakuja ili kutumikiwa bali kutumikia. Aliosha miguu ya rafiki zake. Alikula chakula pamoja na wenye dhambi na kuwashika wakoma. Alitoa maisha yake siku baada ya siku kwa ajili ya watu wake. Na tazama sasa ana sulubishwa na kukataliwa. Alipigiliwa misumari msalabani na tazama anayatoa maisha yake.

Tazama mfalme wako, ametobolewa na damu inatoka miguuni, tunapiga magoti, tukitangaza siku ambayo kila mtu atapiga magoti mbele zake. Tumuangalie huyu mwalimu alivyo haribiwa, na kumuona mfalme wako wa milele, ambaye kwa njia yake vitu vyote viliumbwa. Mtazame huyu Kuhani mkuu amekaa mbinguni akikuombea kwasababu ya dhambi zako kama alivyofanya pale msalabani. Mtazame Yesu. Anga lina giza. Dunia inatetemeka. Miamba ina pasuka. Mwili wake umelala. Ukuu wake umekuwa tupu kutokana na sababu. Hapa yupo Mfalme wako.

Masomo yana andika maneno saba ya Yesu ya mwisho. Tuya tazame.

1. “Bwana, uwasamehe kwasababu hawajui watendalo”. Akiwa ametundikwa msalabani akiwa anavumilia ubaya wa wengine, Yesu aliongea maneno ya Msamaha. Alikiri kwamba hata hawa waliomsulubisha hawakuhusika asilimia zote. Hali hii ya unenyenyekevu wa Yesu unatambua undani wa huruma yake. Inaonesha kwamba hakufa akiwa na hasira au chuki, bali kama sadaka safi. Je, upo tayari kusema maneno haya? Unaweza kuvuta hisia ya watu waliokuumiza ukaita sauti ya Baba awasamehe wote?

2. “Amini, nakuambia utakuwa nami Paradiso”. Ni zawadi ilikuwa kuu namna ghani kuwa karibu na mkombozi wa Ulimwengu, kushiriki katika mateso ya Kristo katika hali halisi. Mwizi huyu alipata zawadi ya kwanza ya kufurahia ukombozi wa Yesu uliopatikana pale msalabani. Yesu anatupa sisi pia uhakika. Anatupatia ukombozi. Anatupatia sisi ukombozi huu tukiwa katikati ya mateso na dhambi zetu. Je, waweza kuisikia sauti yake ikikuita kushiriki katika maisha yake ya milele?

3. “Mama, tazama mwanao”. Hapa, Yesu kwa kufa msalabani anamkabidhi Mama yake mzazi kwa Yohane, alimkabidhi kwa kila mmoja wetu. Umoja wetu na Yesu unatufanya tuwe watu katika familia yake, na hivyo, watoto wa Mama yake mwenyewe. Je, unamkubali mama wa Yesu kama Mama yako wa kiroho?

4. “Mungu wangu, Mungu wangu, kwanini umeniacha?”. Yesu hakuwa ameachwa bali aliruhusu kuhisi kuachwa na Baba yake katika hali ya Kibinadamu. Aliruhusu mwenyewe aweze kutambua na kuelewa madhara ya dhambi. Kwahiyo, anatambua kila tunachopitia tukiwa katika uchungu. Na yupo nasi katika majaribu akitusaidia kusonga mbele kwa Imani na kumwamini Baba.

5. “Nina kiu”. Yesu alihisi kiu kwa wakati huo na alihitaji maji ili kupooza, kupoteza kwake maji mwilini. Lakini zaidi ya hayo, aliona kiu kwa ukombozi wa roho zetu. Aliona kiu ya kutuita watoto wake. Aliona kiu ya mapendo yetu. Tuliza kiu yake siku hii ya Ijumaa kuu kwa kumpa mapendo yako.

6. “Baba, mikononi Mwako naiweka roho yangu”. Haya ni maneno ya kujikabidhi kwa Mungu kabisa. Kujikabidhi maana yake, Mungu ndiye anaye endesha yote. Maana yake kuachia mapenzi yetu na kuruhusu mapenzi ya Mungu yatawale. Na ina maana kwamba Mungu ameahidi kukubali kujikabidhi kwetu na kutuongoza kwenye mpango wake mkamilifu aliyo tuandalia.

7. “Yametimia” kutimia maana yake nini? Hii ni moja wapo ya maneno ya Yesu yanayo toa maana kwamba utume wake wa ukombozi wa dunia umetimia. Ina maana kwamba upendo wake wa sadaka aliyo itoa kwa wote. Kifo chake, tunacho kikumbuka leo, ni sadaka kamili inayo ondoa dhambi za wote. Ni zawadi iliyoje!

Tumezoea kuiona sadaka hii msalabani. Tunaona zawadi hii daima tunapo utazama msalaba. Lakini ni vizuri kutambua kwamba kuzoea kwetu misalaba daima inaweza kutufanya tukashindwa kuona sadaka hii juu ya msalaba. Ni rahisi kusahau kile ambacho Yesu alitufanyia. Tunaomba tendo hili Takatifu la Kimungu lizame ndani ya mioyo yetu. Kutambua sadaka ya Yesu alioitoa pale msalabani itatufanya sisi tupende kama yeye alivyo penda. Itatusadia kuwapenda wale waliotuumiza na kutuchukia. Upendo wake ni Kamili. Ni wa ukarimu wa kupita maelezo.

Sala:
Bwana, ninajua umeona kiu ya roho yangu. Ulimalizia kile ambacho ulianzisha kwa kufa juu ya msalaba kwa ajili ya ukombozi wa ulimwengu. Nisaidie nitambue upendo wako na kuukubali katika maisha yangu. Ninakushukuru , Bwana mpendwa kwa zawadi ya damu yako Takatifu, iliomwagika kwa ukombozi wa Ulimwengu. Bwana, ninakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni