Jumatatu, Machi 26, 2018
Jumatatu, Machi 26, 2018
Juma Kuu
Isa 42: 1-7;
Zab 27: 1-3, 13-14;
Yn 12: 1-11.
HARUFU NZURI YA UPENDO!
Upendo haujui mipaka. Leo, Maria anafanya kitu ambacho ni upendo pekee waweza kufanya. Alichukua kitu cha thamani kubwa kabisa alichokuwa nacho, alichukuwa mafuta na kumpaka Yesu miguu. Kitendo cha Maria kilisukumwa na kitu kimoja tu, tena kimoja tu, Upendo wake kwa Yesu na shukrani kwa huruma ya Mungu. Ilikuwa pia muhimu tena kwamba, Maria alimpangusa Yesu miguu kwa nywele zake, wakati nywele zuri zilizo wekwa vizuri huonyesha utu wa mwanamke kipindi hicho.
Kawaida mwanamke alijisikia fahari kwa nywele zake, ambazo zilichukuliwa kama kivutio, na kama mmoja nywele zake hazikuwa vizuri au kuharibika basi alionekana kama asiye na bahati, au anakosa thamani. Kwakutumia nywele zake kupangusa miguu ya Yesu, Maria alionyesha hali yake ya kujishusha na utayari wake wa kumtumikia Kristo. Maria ni mkarimu na ni mfano wa mfuasi mwema. Anafanya kitu ambacho Yesu angefanya baadae……kuwaosha miguu wafuasi wake.
Yesu hakuwa mbinafsi kwa upendo wake kwetu sisi. Kwa kukubali kupakwa mafuta na Maria Yesu anatukumbusha kitu ambacho tunapaswa kutenda. Tunapaswa kumwabudu, kumheshimu na kumfanya kuwa kiini cha maisha yetu. Tunapaswa kunyenyekea mbele zake na kumtumikia. Si kwasababu yeye anataka tufanye vile tu, bali sisi tunapaswa tufanya vile. Kumheshimu kwa unyenyekevu na upendo ndicho tunacho hitaji kufanya kwasababu ya utakatifu wetu na furaha yetu. Yesu alitambua hili, hivyo anamsifu Maria kwa upendo huu. Kitendo hichi kinatukumbusha sisi pia kufanya vile vile. Kinataka tumtazame Yesu na kumfanya kiini cha kumtukuza na Upendo. Inatualika kuweka kila kazi yetu kwa Yesu (ambayo inawakilishwa na yale Marahamu, mshahara wa siku 300). Hakuna kitu ambacho ni cha gharama sana kwa Yesu. Hakuna chenye thamani kubwa kama Kumwabudu Yesu.
Injili inaeleza kwamba, nyumba yote ilijazwa harufu nzuri ya marashi aliopakwa Yesu. Alichofanya Maria kinaleta harufu nzuri ya furaha kila mahali, ni kama siku chache zijazo tutakapo muona Yesu akituonesha upendo wake wa hali ya juu kwa kutoa kilicho chema kabisa alichokuwa nacho, ambacho ni kutoa damu yake kwaajili yetu na kutupa Roho wake Mtakatifu. Tunapata mfano wa upendo ndani ya Maria na ndani ya Yesu, tuombe pia maisha yetu yatoe harufu nzuri ya upendo wa Yesu.
Sala:
Bwana, ninaomba nifuate mfano wa huyu mwanamke mtakatifu, maria. Bwana mpendwa, hakuna kitu kwenye maisha chenye thamani kama wewe na majitoleo yangu kwako. Ninaomba unitue kwako Ee Yesu, ninyenyekeshe mbele ya utukufu wako nisaidie niweze kupenda na kukuabudu kwa moyo wangu wote. Yesu, nakuamini wewe.
Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni