Jumanne. 21 Mei. 2024

Tafakari

Jumamosi, Juni 25, 2016

Jumamosi, Juni, 25, 2016,
Juma la 12 la Mwaka wa Kanisa


Omb 2: 2, 10-14, 18-19;
Zab 74: 1-7, 20-21;
Mt 8: 5-17


KILIO CHA SALA!!

Masomo yetu ya leo yanatuonesha aina mbili za kilio cha moyo. Kilio cha kwanza ni Kilio cha Waisrael katika hali ya maombolezo, na cha pili ni kilio cha pili cha jemedari katika Injili. Vyote vinamuelekea Mungu wakiwa katika hali ya huzuni. Vilio hivi vyote ni sala ya kumuomba Bwana aje kuwaponya tena, aje apooze tena roho zao zilizo kata tamaa, na kuwakinga na maadui.

Kilio cha kwanza kipo katika hali ya mateso na woga. Mfalme wa Babiloni ameiteka Yerusalemu na aliwachukuwa mateka watu maelfu kutoka Yerusalemu. Wote waliobaki waliishi katika hali ya uharibifu na kutengwa. Waliteseka kuhusu chakula na matumizi yao muhimu.

Kilio cha pili ni kile cha jemedari, alikuwa mpagani. Anakuja kwa Yesu kuomba uponyaja wa mtumishi wake. Imani yake ilikuwa kubwa kuliko ya Myahudi yeyote. Alijua na kutambua kwamba Yesu anauwezo wakuamuru kila kitu kitendeke kama yeye alivyokuwa na uwezo wakuwaamuru watumishi waliokuwa chini yake. Lakini pia alitambua nguvu na uwezo wa Yesu ni wa juu kuliko wake. Alitambua kabisa ilitosha kabisa kwa Yesu kusema neno tu hata bila ya kutembelea nyumbani kwake. Hakuna anyeachwa na mkono wa uponyaji wa Yesu. Yeye yupo karibu na wote, hasa kwa wale wanomhitaji na wanaoteseka, kwasababu katika hali ya mateso yao wanamlilia yeye na kilio chao ni cha uaminifu na kweli na Imani yao kubwa wameiweka kwa Mungu kama tumaini lao.

Sisi nasi tuige mfano huu wakuwa na Imani kwa Yesu, nyakati zote za maisha yetu, tusisubiri tuu tunapatwe na shinda ndio tumkumbuke Mungu. Nyakati zote ziwe za furaha na uchungu Yesu awe ndiye dereva wa maisha yetu yote. Tujikabidhi kwake, Imani yetu, akili yetu na moyo wetu na vyote tulivyo navyo viongozwe na Yesu.

Sala: Bwana sikiliza kilio cha moyo wangu, uniponye mimi, unifanye upya tena na unipe wokovu wako. Amina .

Maoni


Ingia utoe maoni