Jumatano. 27 Novemba. 2024

Tafakari

Jumatatu, Machi 12, 2018

Jumatatu, Machi 12, 2018
Juma la 4 la Kwaresima

Isa 65: 17-21;
Zab 29: 2, 4-6, 11-13;
Yn 4: 43-54.


IMANI KWA YESU
Leo, tunamwona Jemedari anamwomba Yesu kwa ajili ya uhai wa mtoto wake. Anaweka Imani kamili kabisa kwa Yesu. Anadhihirisha Imani yake kwa Yesu. Wakati Yesu alivyosema “waweza kwenda, mtoto wako yu mzima” bila hata kupoteza dakika moja huyu Jemedari anaondoka. Hili linaonesha Imani yake kamili kwa Yesu. Baada ya Yesu kusema mtoto wa huyu Jemedari alipona. Huyu jemedari anashuhudia muujiza. Anapokea kadiri ya Imani yake.

Kitu cha kuvutia cha kugundua katika Injili hii ni utofauti wa maneno ya Yesu. Kwanza kabisa, inaonekana kama Yesu amekasirika aliposema, “bila watu kuona ishara na miujiza, hamuamini”. Lakini mara moja anamponya kijana wa jemedari kwa kumwambia, “Mwanao atakuwa mzima”. Je, kwanini kuna utufatui katika maeneno haya ya Yesu na matendo yake? Yesu anatambua kwamba watu wengi wana Imani dhaifu. Antambua pia ishara na miujiza inasaidia watu wakati mwingine waweze kuamini. Lakini kilele cha malengo ya Yesu haikuwa kwa sababu ya kuponya mwili.

Leo hii dunia imetawaliwa na ugonjwa wa kimwili, kisaikologia na kiroho. Watu wanaenda kutoka sehemu moja hadi nyingine kwenda kutafuta msaada. Lakini je, tunaenda kwa Yesu yeye ambaye ni mponyaji wa Kimungu, ambaye haponyi tu mwili bali roho pia? Je, tuna Imani kama huyu jemedari?

Sala:
Bwana, tafadhali ongeza Imani yangu. Ninakuomba nikuone wewe ukitenda katika maisha yangu, na nisaidie niweze kutambua upendo wako mkamilifu kwa kila kitu. Ninapo kuona wewe ukitenda katika maisha yangu, nisaidie niweze kuutambua kwa hakika kabisa, upendo wakomkamilifu.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni