Ijumaa, Machi 09, 2018
Ijumaa, Machi 9, 2018,
Juma la 3 la Kwaresima
Hos 14:2-10;
Zab 81:6-11,14,17;
Mk 12:28-34
CHAGUA KUMPENDA MUNGU!
Mwandishi alimuuliza Yesu, “ni amri ipi iliyokuu?” na Yesu akajibu ni “Upendo”. Upendo tunao ufahamu na kuhisi katika maisha ni “hali ya kujisikia/kuhisi kutoka ndani mwetu”; hisia, au hali ya kujisikia tunayo ilinganisha na vitu tulivyopokea au kutamani. Katika hali fulani vitu na watu huongoza upendo wetu.
Lakini, anachosema Yesu kuhusu “upendo” ni kitu kingine tofauti. Huu ni upendo ambao tunaweza kuumudu, tunao amua kuutoa. Mungu haitaji upendo wetu ili yeye aweze kuishi. Lakini ameamua kutupatia maisha. Hii si kwasababu anatuhitaji sisi, bali kwasababu anapenda kuutoa. Hii ndio maana ya upendo wa Mungu usio na masharti. Anachotaka Mungu kutoka kwetu ni kuchagua kumpenda yeye kama yeye alivyo chagua kutupenda sisi. Na tunapo fanya hivyo tunapokea upendo wake zaidi, kwani tunabaki katika upendo wake. Kwahiyo, leo tuchague kumpenda Mungu kwa akili zetu zote, na hapo hatutakuwa mbali na ufalme wake.
Hatua ya kwanza katika kumpenda Mungu ni kutaka kumfahamu. Hii ina maana tunapaswa kutafuta jinsi ya kumfahamu, na kutaka kumuelewa na kumwamini Mungu na yote yaliyo funuliwa kwetu kuhusu yeye. Ina maana tumeamua kujikita katika kuingia kufahamu mafumbo ya maisha ya Mungu, hasa kwa njia ya Maandiko Matakatifu na kwa njia ya ufunuo wa mafundisho ya Kanisa katika historia ya Kanisa. Pili, tunaingia katika undani kwa kufuata njia zake. Jambo hili la uhuru kamili linapaswa kufuata akili yetu kuhusu yeye na kuwa kitendo cha Imani kwake. Tatu, tunapo ingia katika kutaka kuyaelewa mafumbo ya maisha ya Kimungu na kuchagua kumwamini na yote aliyo tufunulia, tutaona maisha yetu yatabadilika. Njia maalumu itakayo badilika ni kwamba tuta tamani kuwa na Mungu na kufanya mapenzi yake katika maisha yetu, tuta tamani kumtafuta zaidi, tutapata furaha kwa kumfuata na tuta tambua kuwa upendo wa roho yetu kama wanadamu utazama katika upendo wake na katika njia yake. Tafakari ni mara ngapi umetamani kumfahamu Yesu na kutaka kufahamu yote aliyo tufunulia.
Sala:
Bwana, ninaomba niwe mwaminifu katika kujikita kwangu ili niweze kukufahamu zaidi na kufahamu ukweli wa utukufu wa maisha yako. Ninakushukuru kwa yote ulionifunulia mimi na ninajitolea maisha yangu, leo, katika harakati za kufahamu maisha yako na ufunuo wako. Yesu nakuamini wewe.
Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni