Jumatano. 27 Novemba. 2024

Tafakari

Jumatatu, Machi 05, 2018

JUMATATU, JUMA LA 3 LA KWARESIMA;
MACHI 05, 2018

2Fal 5:1–15;
Zab 42:2–3; 43:3;
LK 4: 24–30.

KUINGIA KATIKA MAPENDO NA YESU!
Ni wiki ya 3 ya kipindi cha Kwaresima, karibia nusu safari ya kipindi chetu cha Kwaresima. Upinzani juu ya Yesu na hao walio karibu naye kumpinga unazidi kukuwa. Yesu ni nabii, akitenganisha kati ya mema na mabaya, na ni nani aliye karibu naye au nani aliye mbali na ufalme aliouleta? Ni kipindi cha kufanya uchaguzi, kuitwa na kubadilika. Tunapaswa tusimame na Yesu.

Yesu anarejea habari inayo husiana na kitabu cha 2 cha Wafalme. Mfalme Aram alivyomtuma Naaman akiwa na barua akiwa na vipande kumi vya silva, vipande elfu 6 vya dhahabu, na nguo za maridadi, akiomba amponye ukoma wake. Mfalme wa Israeli alipokea barua na kurarua nguo yake, akidhani kwamba Mfalme Aram anamtaka uadui. Elisha alivyosikia kuhusu habari za Mfalme kuchana nguo yake, aliamuru amtume Naaman kwake aende na kumuonesha matendo ya Mungu, ili Wafalme na watu wote waweze kutambua kwamba yupo Mungu katika Israeli. Naaman alitii na kwenda katika nyumba ya Elisha. Pale anaambiwa akajichovye mara saba katika mto Yordani ili apone. Naaman anapatwa na hasira. Lakini mtumishi wake alifikiri pamoja naye. Hapo anatii sauti ya Elisha na hapo nyama yake inakuwa kama ya mtoto mdogo. “Naaman anakiri imani yake moja kwa moja “Hakika natambua kwa hakika hakuna Mungu duniani kote, isipokuwa Israeli”.

Katika Injili ya leo, Yesu anawakumbusha kwamba hakuna nabii katika Israeli aliyetokea kukubaliwa nyumbani kwake mwenyewe. Umati unakasirishwa na unataka kumwangamiza Yesu. Wakati alishasema vizuri kuhusu kuwaseta huru wafungwa na kuwapa nguvu waliopondeka moyo hawakuwa tayari kusikiliza sauti yake na kutubu. Mara nyingi majibu yetu yanaweza kufanana na haya ya umati. Sisi tulisafishwa dhambi zetu tulivyompokea hapo mwanzo na tukaona huruma yake. Na hivyo tunavyokaribia karibu zaidi na Mungu, Roho Mtakatifu anatuonesha sehemu ambazo hatukuwa wazi kwake. Na mara nyingi tunaweza kuishia kumkataa Yesu na kutaka kukimbia. Mungu anahitaji kile kilicho cha muhimu kwetu. Mtafute yeye, sikia neno lake, na ingia katika mapendo na Yesu tena!

Sala:
Bwana, ninajitoa mwenyewe kwako. Ingia katika maisha yangu na yafanye upya kwa mapendo yako. Ninaomba pia nitoe upendo wako kwa wengine.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni